Rais Samia akemea mlolongo mrefu wa viza Tanzania

August 15, 2022 2:36 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Aseme mlolongo huo unapunguza idadi ya watalii na wawekezaji.
  • Awaonya askari wasiowaadilifu kuacha tabia hiyo mara moja.

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Idara ya Uhamiaji kupunguza mlolongo mrefu unaotumika kutoa viza na vibali vya makazi kwa wageni wanaoingia nchini ili kuongeza idadi ya watalii na wawekezaji.

Agizo hilo la mkuu wa nchi limekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko juu ya mchakato mrefu wa kupata viza na vibali vya makazi kwa wageni wanaoingia nchini, hatua inayozorotesha juhudi za Serikali za kuvutia wawekezaji na watalii ili kukuza uchumi. 

Rais Samia, aliyekuwa akihitimisha mafunzo ya awali ya askari wa uhamiaji kwenye Chuo Cha Uhamiaji Boma Kichakamiba mkoani Tanga leo Agosti 15, amesema ucheleweshwaji wa viza unachangia kupoteza wawekezaji na wageni wanaotaka kuingia nchini.

“Ningeomba sana punguzeni urasimu kwenye aina zote za viza na kwa sababu sasa hivi mnatumia teknolojia hakuna sababu ya kuchelewesha viza kwa wale wote ambao hawana tatizo kuingia nchini kwetu,” amesema Rais Samia.

Kwa muda mrefu baadhi ya wageni wamekua wakilalamikia mlolongo mrefu wa kupata viza ikiwemo muda mrefu wa siku 10 wanazotakiwa kusubiri kabla ya kupewa majibu ya maombi ya viza zao.


Zinazohusiana:


Askari wa uhamiaji  wasio waadilifu waonywa

Katika hotuba hiyo, Rais Samia amewaonya askari wa uhamiaji wasio waaadilifu, wanaohujumu fedha za vibali vya makazi na viza na kutaka hatua zichukuliwe kwa wote wanaofanya uhujumu huo.

Rais Samia amesema kupitia utafiti mdogo uliofanyika kwenye mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar wamebaini upotevu mkubwa wa fedha unaofanywa na maafisa uhamiaji na kutaka vitendo hivyo vikomeshwe.

“Wale wote waliohusika na mambo yale washughulikiwe,” ameongeza Rais.

Ili kukomesha vitendo vya vya rushwa na unyanyasaji wa raia wa kigeni unaofanywa  kwa maafisa wahamiaji, Rais Samia amesema kuwa kuna haja maafisa hao wanaofanya vitendo hivyo  kurudi tena kwenye mafunzo ili wakumbushwe wajibu wao.

Aidha Rais Samia amesema Serikali imetoa fedha ili maafisa wa vikosi vyote vya Tanzania wapate mafu

nzo yatakayo wawezesha kuongeza ufanisi kwenye vituo vyao vya kazi.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW