Ushindani: Kampuni za simu kutengeneza magari ya umeme

August 26, 2022 11:23 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Kampuni ya Xiaomi itaanza kutengeneza magari hayo mwaka ujao.
  • Itaunga na kampuni za Apple na  Foxconn zinatengeneza magari hayo.
  • Lengo ni kutoa ushindani, kutunza mazingira na kuongeza kipato.

Dar es Salaam. Kampuni ya kutengeneza simu janja ya Xiaomi ya nchini China inatarajia kuanza kutengeneza magari ya umeme ifikapo mwaka 2023 ikiwa ni hatua ya kuongeza wigo wa mapato na ushindani katika teknolojia mpya zinazotunza mazingira.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Bloomberg, kampuni hiyo iko kwenye mazungumzo na kampuni ya  utengenezaji wa magari ya BluePark New Energy Technology ya Beijing ili kushirikiana katika kutengeneza magari hayo. 

Kampuni  hizo zinaangalia pia uwezekano wa Xiaomi kununua hisa katika mtambo wa Beijing Hyundai namba 2, ambao una leseni kamili ya kutengeneza magari nchini China, wakati ikikabiliwa na ucheleweshaji wa kupata leseni ya kutengeneza magari peke yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Xiaomi Lei Jun alisema mwaka jana kuwa kampuni hiyo itaanza uzalishaji mkubwa wa gari lake la umeme la ndani katika nusu ya kwanza ya 2023. 

Xiaomi imesema itaingia katika sekta ya ushindani wa magari ya umeme na kutoa changamoto kwa kampuni za teknolojia zilizopo na mpya.


Soma zaidi:

Kampuni hiyo imejipanga kutengeneza magari hayo kwa uzalishaji mkubwa katika nusu ya kwanza ya 2024. Mapema mwaka huu, ilianza ujenzi wa kiwanda chake cha kwanza cha magari huko Beijing.

Ushirikiano huo utamruhusu mwanzilishi mwenza wa Xiaomi Lei Jun kutimiza ahadi ya kuwekeza takriban Sh33 trilioni kwa muongo mmoja kutengeneza magari yenye chapa ya Xiaomi ifikapo 2024.

China imekuwa ikiongeza uchunguzi wa kampuni za umeme wa magari baada ya idadi kubwa ya kampuni kukimbilia katika sekta hiyo, zikishawishiwa na punguzo la ushuru na ruzuku ya Serikali.

Kampuni nyingine za simu zinazojihushisha na utengenezaji wa magari ya umeme ni pamoja na Apple inayotengeenza simu za iPhone, Foxconn na BBK Group kupitia kampuni za  simu janja za Oppo, OnePlus, Vivo, na Realme.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV