Hapana: Chanjo ya Uviko-19 haisababishi homa ya monkeypox

October 21, 2022 11:46 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Watu waaswa kutohusianisha uwiano wa vitu na usababishi.
  • Tafiti za kisayansi zathibitisha chanjo za Uviko-19 hazisababishi homa ya nyani.

Dar es Salaam. Dunia inaendelea kukabiliwa na mfululizo wa milipuko ya magonjwa ambayo yamekuwa na athari hasi kiuchumi, kijamii na hata kisiasa.

Wakati mataifa mbalimbali yakianza kupata ahueni kutokana na athari za Uviko-19,baadhi ya mataifa yameripoti visa vya maambukizi ya homa ya nyani (monkeypox) na kuibua hofu juu ya madhara yanayoweza kutokea.

Kuibuka kwa monkeypox kumekuja sambamba na uzushi kwamba huenda ugonjwa huo unasababishwa na chanjo ya Uviko-19 aina ya Pfizer kutokana na ugonjwa huo kuripotiwa kwa wingi katika maeneo ambayo chanjo hiyo imetolewa.

Hata hivyo, wataalamu wa afya kutoka Shirika la Afya la kimataifa (WHO) wamekanusha uzushi huo na kufafanua kuwa uzushi huo umechagizwa na magonjwa yote mawili kuibuka kwa wakati mmoja.


Soma zaidi:


“Vitu viwili vinapotokea kwa wakati mmoja hudhaniwa kwamba kimojawapo ndio kimesababisha kingine kutokea, watu wanahusianisha chanjo ya Pfizer na homa ya nyani, hakuna uthibitisho wa kisayansi kwamba magonjwa haya yanahusiana wala kama chanjo ya Pfizer inasababisha homa hiyo, ” imeeleza WHO.

WHO imesema vitu vinaweza kuwiana lakini visihusiane na ili kuthibitisha kama vinahusiana ni lazima ufanyike utafiti wa kisayansi ambao unaonesha chanjo za Uviko-19 inasababisha homa ya nyani ambapo matokeo ya utafiti hayajathibitisha uzushi huo.

Monkeypox  ni ugonjwa unaoambukiza kutoka kwa wanyama kama nyani na panya kwenda kwa binadamu na uligunduliwa mara ya kwanza mwaka 1958 na kutokomezwa kabisa mwaka 1980.

Hata hivyo, ugonjwa huo umekuwa ukijirudia mara kwa mara kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa(CDC) cha nchini Marekani hadi leo Octoba 20,2022 vimethibitishwa jumla ya visa 74,785 pamoja na vifo 32.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV