Mwelekeo mpya mapambano magonjwa ya milipuko duniani

November 22, 2022 12:31 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanasayansi kujichimbia kufuatilia vimelea vya magonjwa hayo.
  • Magonjwa kama Uviko-19, Ebola na Marbug kupewa kipaumbele.  

Dar es salaam. Wakati mataifa mbalimbali duniani yakiendelea  kukabiliana na magonjwa ya milipuko ambayo yamesababisha athari nyingi kiuchumi na kijamii ikiwemo Uviko-19 na Ebola, wanasayansi wanafikiria kuja na suluhu ya kuepusha kabisa magonjwa hayo kwa siku za usoni.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Shirika la Afya Duniani (WHO) jana Jumatatu Novemba 21, 2022, shirika hilo lipo mbioni kuzindua mchakato wa kufuatilia vimelea ambavyo vinaweza kusababisha magonjwa ya milipuko.

Ufuatiliaji huo utafanywa na jopo la wanasayansi zaidi ya 300 ambao watafuatilia familia za bakteria na virusi 25 na kisha watapendekeza ni vimelea vipi vipewe kipaumbele zaidi.


Soma zaidi:


Mchakato huo utahusisha vigezo vya kisayansi vinavyohusiana na athari za kijamii na kiuchumi ambapo unatarajiwa utachochea maendeleo ya tafiti katika upatikanaji wa tiba pamoja na chanjo.

“Ni muhimu kuwa na mchakato huu hususan linapotokea janga linalohitaji majibu ya haraka kama Uviko-19, isingekuwa rahisi kupambana nao kwa haraka kama kusingekuwa na hatua kama hizi,” anasema Dk Michael Ryan, Mkurugenzi wa Mpango wa Dharura wa WHO.

Magonjwa kama Ebola, Uviko-19, Marbug, homa ya Lassa, homa ya bonde la ufa pamoja na zika ni miongoni mwa maradhi yaliyopo katika orodha ya magonjwa yatakayopewa kipaumbele katika utafiti huo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV