Watatu washikiliwa na polisi mauaji ya mhadhiri SAUT

December 2, 2022 7:44 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni Hamida Mussa aliyenyongwa Novemba 28 mkoani Mwanza.
  • Anayedaiwa kumuua ni dada wa kazi aliyekuwa akiishi naye.
  • Watu watatu wahusishwa na mauaji hayo.

Mwanza. Jeshi la polisi linawashikilia watatu watatu kwa tuhuma za kumuua Hamida Mussa, Mhadhili wa Chuo Kikuu cha St Augustine (SAUT) tawi la Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Wilbroad Mtafungwa amesema tukio hilo limetokea Novemba 28 mwaka huu katika mtaa wa Buzuruga wilayani Ilemela.

Marehemu Hamida aliuawa kwa kunyongwa shingoni na mtandio akiwa nyumbani kwake. Tukio hilo linadaiwa kutekelezwa na watu watatu: Sara Mwendesha, Mashiri Benard na Tabu Selemani.

“Inadaiwa Novemba 28 hadi 29 ndugu na marafiki wa marehemu walikuwa wakifanya mawasiliano na ndugu yao bila mafanikio kwani simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa hivyo kuingiwa na wasiwasi.

“Waliamua kutoa taarifa kituo cha polisi, na baada ya polisi kushirikiana na viongozi wa serikali ya mtaa walifika kwenye makazi ya marehemu na kukuta mlango ukiwa umefungwa huku nyumba ikiwa na ukimya,” amesema Kamanda Mtafungwa.

Marehemu alikuwa akiishi na binti wa kazi aliyefahamika kwa jina moja la Sara (15) na kwamba baada ya polisi kuvunja mlango walikuta mwili wa marehemu ukiwa sakafuni na binti huyo akiwa ametoweka kusikojulikana.

“Polisi walianza kufanya ufuatiliaji kumsaka binti huyo na walifanikiwa kumkamata stendi ya mabasi wilayani Misungwi akiwa anaelekea kwao kijiji cha Ishokelahela ambapo alikamatwa akiwa na vitu mbalimbali mali ya marehemu alivyovichukua baada ya kufanya tukio la mauaj,” amesema Mtafungwa.

Vitu alivyokutwa navyo binti huyo ni pamoja na simu aina ya Tecno, kitambulisho cha kazi, kadi ya bima ya afya, kadi ya benki ya CRDB, kadi ya mpiga kura, kadi ya Eco water, kadi ya posta, kitabu kidogo cha kutunzia kumbukumbu vyote vikiwa na majina ya marehemu.

Pia mtuhumiwa amekutwa akiwa na pete mbili rangi ya dhahabu, mkufu mmoja rangi ya dhahabu, viatu, sabuni ya unga kilogramu 15, hereni moja, viberiti bunda 14, sabuni aina ya B29 box mbili na sukari kilogramu mbili.

Vitu vingine ni nmabegi matatu makubwa na moja dogo la mgongoni yote yakiwa na nguo mbalimbali za marehemu pamoja na nguo za Hamida Petro ambaye ni mjukuu wa marehemu.

Baada ya mtuhumiwa kuhojiwa kwa kina, ameieleza polisi kuwa vitu hivyo vyote alivichukua kutoka nyumbani kwa marehemu baada ya kuwa amemuuwa kwa kumnyonga shingo kisha kujifungia naye ndani na ilipofika tarehe 29 alitoroka akiacha amemfungia kwa ndani.

Baada ya kutendewa unyama huo, mtuhumiwa aliondoka na vitu vya marehemu livyokamatwa navyo hadi Misungwi ambako alimpigia simu mama yake mzazi aitwaye Bashiri Benard anayeishi kijiji cha Ishokela ili ampatie baadhi ya vitu kama zawadi, mama huyo alifika na kupatiwa baadhi ya vitu hivyo nakurejea kijijini.

“Mtuhumiwa ameendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kueleza kuwa aliamua kufanya tukio hilo kwasababu ya hasira kwa kuwa marehemu alikuwa akimkaripia anapofanya makosa hapo nyumbani, kumpiga makofi na kumpa kazi ngumu,” amesema Mtafungwa.

Hata hivyo, ameeleza kuwa vitu vingine alikwenda kuvihifadhi nyumbani kwa Tabu Seleman ambaye ni shemeji yake aishiye Misungwi.

Watuhumiwa wote watatu wanaendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV