Necta: Hatujatangaza matokeo ya kidato cha nne 2022

January 26, 2023 5:32 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wananchi watakiwa kupuuzia taarifa hizo
  • Necta yasema matokeo yatatangazwa muda wowote yatapokuwa tayari.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limewataka wananchi kupuuzia taarifa zinazosambazwa mtandaoni kuwa baraza hilo limetoa matokeo ya mitihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2022.

Necta imetoa taarifa hizo leo Januari 25, 2023 kupitia taarifa ya  Afisa Habari na Mawasiliano wake, John Nchimbi ambapo imejulisha umma kuwa taarifa  hizo zinazosambazwa kuhusu baraza hilo si za kweli.

“Baraza linapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hizo ni za uongo na zinalenga kupotosha umma na kuleta taharuki,” amesema Nchimbi katika taarifa hiyo.


Soma zaidi


Taarifa hiyo imefafanua zaidi kuwa matokeo ya kidato cha nne 2022 yatatangazwa rasmi na baraza hilo kupitia vyombo vya habari muda wowote yatakapokuwa tayari.

Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne kwa mwaka 2022 ulianza kufanyika Novemba 14 na kumalizika Disemba 1, 2022 huku watahiniwa 566,840 kutoka shule 5,212 wakisajiliwa kufanya mtihani huo.

Kwa kawaida matokeo ya mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne hutangazwa Januari au Februari.

/
No matches found for this filter
30 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV