Necta yazidi kuwafyeka wadanganyifu mtihani kidato cha sita Tanzania

July 5, 2022 12:02 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanafunzi waliofutiwa mitihani kwa udanganyifu wapungua kwa asilimia 52
  • Necta yapongeza kamati za mitihani kwa kuziba mianya.
  • Waliozuiwa matokeo yao kwa sababu ya maradhi kurudia mtihani Mei 2023.

Dar es Salaam. Watahiniwa 15 wamefutiwa matokeo yao ya mtihani wa kidato cha sita Mwaka 2022 kutokana na vitendo vya udanganyifu idadi ambayo imepungua kwa takriban mara mbili ndani ya mwaka mmoja.  

Katika mkutano wake na wanahabari, Naibu Katibu wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) Athumani Amas amesema robo tatu ya watu hao ni watahiniwa wa shule. 

Uamuzi huo wa Necta utawapelekea maumivu watahiniwa hao kwa kuwa sasa utawafanya wakose fursa ya kuendelea na masomo ya juu mwaka huu.

“Baraza la mitihani katika mkutano wake limefuta matokeo yote ya watahiniwa 15, waliobainika kufanya vitendo vya udanganyifu katika mtihani, kati ya watahiniwa hao 13 ni watahiniwa wa shule na wawili ni watahiniwa binafsi,” amesema Amas wakati akitangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita pamoja na ualimu mwaka 2022.  


Soma zaidi:


Katika matokeo ya mwaka 2021, wanafunzi 27 walifutiwa matokeo yao kutokana na vitendo vya udanganyifu. Hii ina maana kuwa angalau mwaka huu idadi ya watahiniwa wadanganyifu imepungua kwa takriban asilimia 52. 

Hata hivyo, bosi huyo wa Necta hakueleza kwa undani vitendo ambavyo wamefanya watoto hao. Miongoni mwa vitendo maarufu vya udanganyifu katika mitihani ni kuingia na karatasi za majibu au simu kwenye chumba cha mtihani au kuangalizia mtihani wa mwenzio. 

Amas ametoa pongezi kwa kamati za uendeshaji wa mitihani kwa kuzingatia na kusimamia kikamilifu sheria na taratibu za uendeshaji mitihani na hivyo kuzuia udanganyifu.

Sanjari na uamuzi huo, baraza hilo lenye makao yake Mikocheni jijini Dar es Salaam, limezuia matokeo ya watahiniwa 21 ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani kwa baadhi ya masomo.

Kwa mujibu wa Amas, watahiniwa husika ambao hawakufanya mitihani hiyo kwa sababu ya maradhi wamepewa fursa ya kufanya mitihani Mei 2023 kama watahiniwa wa shule.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV