Maumivu, ahueni, Latra wakitangaza nauli mpya magari ya abiria

November 27, 2023 2:53 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Zaongezeka kwa Sh100 hadi Sh300 kwa daladala.
  • Ni baada ya wamiliki wa vyombo vya usafiri kupendekeza nauli ziongezeke.
  • Nauli ya wanafunzi yasalia Sh200.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti na Usafiri Ardhini ( Latra) imetangaza nauli mpya za usafiri wa mabasi ya abiria kwa masafa marefu na mafupi jambo linalotoa ahueni kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri na maumivu kwa watumiaji.

Mkurugenzi mkuu wa Latra, Habibu Suluo aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo  Novemba 27, 2023 mkoani Arusha amesema uamuzi wa kupanda kwa nauli hizo umetokana na maamuzi yaliyofanywa na bodi ya mamlaka hiyo Oktoba 25, 2023.

“Bodi ilijiridhisha kuwa bei iliyorejewa zimezingatia mambo ya msingi yatakayofanya huduma iweze kupatikana na watumiaji wa huduma waendelee kumudu nauli hizo,” amesema Suluo.

Itakumbukwa kuwa tangazo hilo  limekuja ikiwa imepita siku kadhaa tangu wamiliki wa mabasi wawasilishe mapendekezo ya kuongezwa kwa nauli kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kupanda kwa bei ya mafuta.

Kwa muda wa miezi mitano mfululizo bei ya mafuta imekuwa ikiendelea kupanda nchini Tanzania ikichangiwa zaidi na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na gharama za usafirishaji.

Bodi ya Latra imetoa siku 14 tangu kutangazwa rasmi kwa nauli hizo katika gazeti la Serikali Novemba 24 mwaka huu kwa wamiliki wa mabasi hayo kukata rufaa ikiwa hawakuridhishwa na baada ya muda huo kupita bei hizo zitaanza kutumika rasmi.

Bei za mabasi yenye safari ndefu kuanzia kilomita 36 hadi 40 zimeongezeka zaidi kutokana na sababu mbalimbali ikwemo kutumia muda mwingi njiani na foleni.Picha CNN

Maumivu kwa wapanda daladala

Suluo amebainisha kuwa kwa safari za daladala zilizokuwa zinafanyika nchini nauli imepanda kwa Sh100 hadi Sh300.

“Kwa safari zile ambazo hazizidi kilomita 10 nauli ya sasa ni Sh500 ule uchambuzi wa kitaalamu wa kikokotoo ni Sh 601na senti 22 hiyo nauli yake itakwenda Sh 600,” amefafanua Suluo.

Kwa waliokuwa wakisafiri kwa kilomita 11 hadi 15 ambapo walikuwa wanalipa Sh550 sasa watalazimika kulipa zaidi hadi Sh700  ikiwa ni ongezeko la asilimia 27 kutoka ile iliyokuwa inatumika awali.

Safari za kilometa 16 hadi 20 nauli itapanda kutoka Sh600 hadi Sh 800, kilomita 21 hadi 25 (kutoka Sh700 hadi Sh900),  kilomita 26 hadi 30 (kutoa 850 hadi 1100), 

Watumiaji waliokuwa wanatumia kilomita 31 hadi 35  sasa watalipa Sh1,300 kutoka Sh1,000 waliyokuwa wanalipa awali huku wale wa kilomita 36 hadi 40  wakitakiwa kulipa Sh1,400 kutoka Sh1100.

Akizungumzia ongezeko hilo kwa safari zenye umbali mrefu Suluo amesema bei hizo ni kubwa kutokana na muda ambao vyombo hivyo vinautumia vikiwa njiani.

“Hii ndo ile ukiangalia idadi ya safari yani mtu anakuwa na foleni kwa muda mrefu…nikupe Sh1,400 alafu usinifikishe safari yangu ya kilomita 40 itakuwa shida,” ameongeza Suluo.


Soma zaidi:Hatari inayowakabili wauzaji, watumiaji mafuta ya vibaba, mkoani Mwanza


Ahueni maumivu kwa mabasi ya masafa marefu 

Kwa mabasi ya masafa marefu nauli zimeongezeka kulingana na aina ya barabara, daraja la basi pamoja na umbali basi linapoenda jambo linalotoa ahueni kwa wamiliki wa vyombo waliowasilisha mapendekezo ya kuongezeka kwa bei hizo mapema mwezi Oktoba mwaka huu.  

Kwa mabasi ya masafa marefu daraja la kawaida litakalopita njia ya lami nauli imeongenza hadi Sh48.47 kwa kilomita moja kutoka Sh41.29 iliyokuwa ikitumika awali huku njia ya vumbi ikiongezeka kwa Sh53.32  kutoka Sh51.61 iliyotumika awali.

Wale wanaopanda daraja la kati wajiandae kutoboa mifuko zaidi kwani nauli imepanda kwa  asilimia 19.27 kutoka Sh56.88 kwa kilomita1 hadi 67.84. 

Kiongozi huyo amebainisha kuwa nauli hizo zilizotangazwa leo zinajumuisha tozo za Latra zinazopaswa kulipwa na wamiliki wa vyombo hivyo huku akisistiza nauli ya wanafunzi kusalia kuwa Sh200.

“Nauli ya wanafunzi inaendelea kubaki Sh200 kwa kila wanafunzi kwa safari tulizoziataja…hapa inawezekana msituelewe lakini hawa wazazi ndio tayari washachangia hapo juu,” amefafanua Suluo.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV