Wakulima wa korosho kupigwa jeki na ushuru wa mapato ya mauzo ya nje

June 29, 2022 2:08 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya mjadala mkali kati ya  mawaziri na mbunge kutoka mikoa ya kusini.
  • Fedha hizo zitakwenda kutoa ruzuku pembejeo za korosho kupitia Wizara ya Kilimo.

Dar es Salaam. Huenda wakulima wa korosho nchini Tanzania wakapata neema katika msimu ujao wa kilimo na kuongeza uzalishaji wa zao hilo mara baada ya Serikali kuridhia asilimia 50 ya ushuru wa mauzo ya nje ya nchi kwenda kutumika kama ruzuku kwenye pembejeo za korosho.

Serikali imekubali pendekezo hilo mara baada ya kuibuka mjadala  mkali kati ya Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba pamoja na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akiwataka  kufanya marekebisho kwenye  sheria ya korosho ili itamke rasmi kuwa asilimia 50 za mauzo ya nje itakwenda kwenye korosho na siyo kilimo kwa ujumla. 

“Hii sheria itamke kabisa kwamba hii pesa inakwenda kutumika kwenye korosho kwa sababu ndiko inakokusanywa kwa hiyo wakubali kuongeza hiki kipengele kama ambavyo ipo kwenye muswada wa mabadiliko…fedha hii ikatumike kwenye pembejeo za korosho,” amesema Mwambe Juni 28, 2022 Bungeni jiijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo ruzuku iliyotolewa na Serikali kwa mwaka 2021/22 imesababisha ongezeko la uzalishaji katika msimu huu wa korosho ambao umefikia tani 238,555.8 sawa na asilimia 85.2 ya lengo la kuzalisha tani 280,000 tofauti na msimu wa 2020/21 ambapo uzalishaji wa zao hilo ulikuwa tani 210,000.

Alipokuwa akijibia marekebisho hayo, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema anakubaliana na marekebisho hayo  ya kwamba fedha hizo zikatumike maalumu kwa ajili ya korosho tu kama alivyopendekeza kwenye marekebisho yake. 

“Niyapokee mawazo mazuri ya mbunge…ili kuielekeza fedha hii ionekane inakwenda moja kwa moja kwenye korosho,” amesema Bashe.


Zinazohusiana:   


Hata hivyo, Serikali imekataa pendekezo la pili la Mwambe ambaye aliitaka Serikali kutenga asilimia 15 ya ushuru wa mauzo ya nje kwa ajili ya maendeleo ya kilimo na asilimia 30 ziende mfuko mkuu. 

Waziri Dk Nchemba alipokuwa akizungumza wakati wa kuhitimisha mjadala huo wa marekebisho ya muswada wa Sheria ya Fedha mwaka 2022 amesema ”sisi tumeweka asilimia 50 inakwenda kwa ajili ya zao la korosho inapitia tu kwenye wizara ya kilimo…lakini pendelezo lake la pili hatukubaliani nalo kwa sababu kuna pesa nyingine ambazo zitafanya kazi hiyo hiyo.”

Mara baada ya Mwambe kuridhia mabadiliko ya Serikali, Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson  amewataka mawaziri wanaohusika wakatengeneze kanuni itakayoelekeza fedha hizo kutumika kwenye korosho katika bunge lijalo la utungaji wa sheria.

Wakulima wa korosho wamekuwa wakipambana kuongeza uzalishaji na kupata masoko ya uhakika ya zao hilo ili kupata tija licha ya kukabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo matumizi ya teknolojia duni na ukosefu wa uhakika wa pembejeo.

Korosho ina umuhimu wake katika maisha ya Watanzania hasa wakulima wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Ruvuma na Tanga kwa kuwa hutegemea zao hilo kujiingizia kipato ambacho hutumika kutunza familia na kusomesha watoto ili kuondokana na umaskini katika jamii.

Pia Bunge limepitisha muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2022 ambapo  Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishasaini itakuwa sheria rasmi.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
25 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV