Mamia wajitokeza kumzika Lowassa, Rais Samia ahimiza kuyaenzi mema aliyoyaacha

February 17, 2024 12:53 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Azikwa kiheshima kwa taratibu za kiserikali, kidini na kimila.
  • Mamia ya wananchi, viongozi wa Serikali wajitokeza kumzika
  • Rais Samia asema ameliachia Taifa mambo makubwa matatu.

Dar es Salaam. Hatimaye mwili wa hayati Edward Lowassa umepumzishwa kwenye  nyumba yake ya milele katika kijiji cha Ngarashi, wilayani Monduli mkoani Arusha ikiwa ni siku saba tangu apoteze maisha Februari 10 mwaka huu.

Maisha ya Hayati Lowassa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kati ya mwaka 2005 hadi 2008 yalikatishwa na maradhi ya muda mrefu  ikiwemo ya kujikunja kwa utumbo na kuiacha familia na watanzania kwenye majonzi.

Leo Februari 17, 2024 saa 6 mchana mwili wa kiongozi huyo umepumzishwa katika nyumba yake ya milele kwa ibada iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, kimila na Serikali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizinguza mara baada ya ratiba za mazishi hayo kukamilika Rais Samia amewarai Watanzania kuyaenzi mema yote yaliyoachwa na kiongozi huyo katika ngazi za kijamii, kidini na kisiasa.

“Yamesemwa mengi kumuhusu mpendwa wetu Edward Lowas, tuedelee kumuenzikwa kuyaishi yale mema aliyoyaamini na kuyasimamia,” amesema Rais Samia.

Familia ya Lowassa ikitoa salamu za mwisho kwa mpendwa wao kabla ya mazishi.Picha|Ikulu Mawasiliano.

Aidha, Rais Samia amewaambia waombolezaji kuwa kati ya  masomo makubwa mabayo kiongozi huyo ameliachai Taifa ni pamoja na  ushupavu, ustahimilivu na ulezi.

“Kwa waliomfahamu Edward Lowasa watakubaliana nami  alikuwa mlezi, kiongozi alyelea na kukuza wanasiasa vijana wengi ambao wananendelea kulitumia Taifa…

…Sifa hii ilimjengea umaruufu na mapenzi kwa makubwa miongooni mwa wengi,” amebainisha Rais Samia.

Mbali na Rais Samia, viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu Dotto Biteko, Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson, mawaziri, manaibu waziri, wabunge na viongozi wengine kutoka vyama vya upinzani.


Zinazohusiana:Dk. Mpango aongoza Watanzania kumuaga Lowassa Dar es Salaam


Azikwa kwa heshima

Kama ilivyo katika mazishi ya  viongozi nwengine wa Serikali mazishi ya Lowassa yalifanyika katika taratibu za kijeshi ikiwemo kupigiwa saluti na mizinga 17 iliyoashiria heshima kwa kiongozi huyo ambaye pia aliwahi kulitumikia Jeshi la Tanzania katika vita ya Tanzania na Uganda.

Kiongozi huyo pia amezikwa kwa kufuata taratibu za kanisa kwa ibada maalum iliyoongozwa na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) kisha kufuatiwa na mazishi ya kimila yaliyoongozwa na Mkuu wa Jamii ya Wamasai Laigwanan Ole kisongo Meijo.

Baada ya taratibu hizo wanafamilia na viongozi wa Serikali walipata nafasi yakutoa heshima zao za mwisho kwa kuweka udongo na taji la maua katika kaburi lake lililosakafiwa kwa viagae vyeussi na kupambwa kwa maua meupe.

Fredrick Lowassa, mtoto wa kwanza wa hayati Lowassa aliyekuwa akizungumza kwa niaba ya familia, amewashukuru wananchi na viongozi wa Serikali  kwa kuwa pamoja na familia hiyo tangu wanauguza mpaka baba yao anapoteza maisha.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV