Majaliwa: Teknolojia itasaidia kukabiliana na rushwa,ubadhirifu nchini

February 15, 2024 11:23 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema ni miongoni mwa maeneo ambayo Serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwa kasi.
  • Waziri Nape ataja nguzo tano zinazoongoza mapinduzi ya Tehama nchini.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, amebainisha kuwa Serikali inapigia chapuo maendeleo ya sayansi na teknolojia katika utoaji wa huduma mbalimbali ikiwemo za kijamii nchini ili kukabiliana na rushwa pamoja na ubadhirifu.

Majaliwa aliyekuwa akizungumza katika ufunguzi wa kongamano la wadau wa teknolojia la ‘Future Ready Summit’ (FRS) leo Februari 15, 2024 amewaambia washiriki kuwa maendeleo ya teknolojia katika utoaji huduma  yatapunguza muda pamoja na watu kuonana ana kwa ana jambo litakalosaidia kuziba mianya ya rushwa.

“Serikali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari inaendelea kuimarisha kuhakikisha kila huduma hapa nchini inatolewa kidijitali…

…na kwa kufanya hivyo tutapunguza rushwa, ubadhirifu, wizi, ili kila mmoja atumie alichonacho kupata huduma anayoitaka kwa gharama ile ile, hatua hii ndiyo ambayo sisi tunaendelea nayo kwa kasi,” amesema Majaliwa.


Soma zaidi:Teknolojia ya kuteketeza taulo za kike (pedi) itakavyookoa mazingira Tanzania


Kauli hiyo ya Waziri Mkuu, inakuja wakati ambao tayari wadau wa maendeleo wamekuwa wakiishauri Serikali kuboresha mifumo ya utoaji huduma kuwa ya kidijiti ili kurahisisha upatikanaji wake kwa kuepusha milolongo mirefu isiyo na lazima.

Miongoni mwa huduma zinazofanyika kidijiti hivi sasa ni pamoja na maombi ya hati ya kusafiria ‘Passport’, pamoja na maombi ya Namba ya Mlipa Kodi (TIN).

Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema ili kufanikisha upatikanaji wa huduma za kidijiti Serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano ikiwemo minara mipya pamoja na kuipandisha hadhi minara kwenda katika teknolojia ya 2G, 3G na 4G.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akisikiliza jambo wakati akitembelea mabanda ya maonyeshokatika kongamano la ‘Future Ready Summit’ jijini Dar es Salaam.Picha|Ofisi ya Waziri Mkuu/Twitter.

Kwa upande wake Waziri wa Habari Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Nape Nnauye, amesema Serikali inandelea kutengeneza msingi imara wa kisheria utakaosaidia upatikanaji, uendelezaji na uanzishaji wa huduma za teknolojia.

“Pale wizarani tumekubaliana na wenzangu tuwe na misingi mitano inayotuongoza, ambayo ni upatikanaji wa huduma, unafuu, ubora, usalama pamoja na matokeo chanya,” amesema Waziri Nape.

Kongamano la FRS limewakutanisha wadau katika sekta ya teknolojia ikiwemo wawekezaji, watunga sera, na wabunifu wa teknolojia kujadili changamoto, fursa pamoja na mikakati ya kuendeleza matumizi ya teknolojia kujiletea maendeleo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV