Serikali, wadau kunusuru wanafunzi 120, 000 dhidi ya udumavu

June 19, 2023 2:06 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni wanafunzi 240 kutoka shule za Kanda ya Ziwa.
  • ni kupitia mradi wa lishe kwa wanafunzi.

Mwanza. Wanafunzi 120,000 kutoka mikoa sita ya kanda ya Ziwa watanufaika na mradi mpya wa lishe unaolenga kuwanusuru na tatizo la udumavu unaotokana na kukosa virutubisho na lishe bora.

Geita, Kagera na Simiyu ni miongoni mwa mikoa iliyopo katika orodha ya mikoa yenye wastani mkubwa wa watoto wenye udumavu nchini ambapo licha ya kuwa na chakula cha kutosha bado udumavu ni wa kiwango kikubwa.

Mradi huo unaotekelezwa na Serikali na wadau wa lishe nchini unalenga kutoa lishe bora kwa  wanafunzi kutoka shule 240 za mikoa ya Mwanza, Geita, Simiyu, Kagera, Shinyanga na Mara ili kuwaepusha na tatizo la udumavu.

Lishe hiyo itahusisha virutubisho mbalimbali ikiwemo madini ya chuma, vitamini B12 na folic asidi. Virutubisho hivyo pia vitaongezwa kwenye vitu vingine kama chumvi, mafuta ya kula na ngano.

Mtaalam wa lishe kutoka Kampuni ya Sanku, Josephine Kimario aliyekuwa akizungumza kwenye mkutano uliokutanisha wasindikaji wa unga wa sembe na dona kutoka mikoa hiyo, amesema wamekuja na mpango wa kuhakikisha tatizo la udumavu linatatuliwa.

“Kutakuwa na shule 40 kila mkoa ambazo wanafunzi watatakiwa kula vyakula vilivyorutubishwa ili kuwakinga na matatizo hayo kwa siku za baadae,” amesema Josephine.


Soma zaidi


Katika mradi huo, jumla ya wazalishaji 850 wameshirikishwa ambao watashiriki kikamilifu kuhakikisha mashine zao zina kifaa maalumu cha kuchanganya unga huo. 

“Mpango ni kufikia nchi nzima lakini sasa tumeanza na kundi la wanafunzi, na kwamba hivi sasa wazalishaji wanauwezo wa kuzalisha unga unaotosheleza watu milioni sita kwa nchi nzima,” amesema Josephine.

Mpaka sasa ni mikoa tisa ambayo inakabiliwa na tatizo la udumavu ikiwemo mikoa ya Njombe, Iringa na Kagera, ambapo Serikali imeweka mikakati kuhakikisha wanatatua tatizo hilo hilo.

Baadhi ya wsindikaji Kanda ya Ziwa  wakipokea maelekezo juu ya namna ya kuchanganya virutubisho katika vyakula vitakavyotumiwa na wanafunzi. Pichal Mariam/ Nukta

Licha ya mikoa hiyo kuongoza kwa udumavu takwimu za Taarifa ya Hali ya Chakula Nchini kwa mwaka 2020/2021 na mwaka 2021/2022 inayotolewa na Wizara ya Kilimo zinaonyesha mikoa hiyo inaongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula. 

Mathalani mkoa wa Kagera ulizalisha tani za chakula 166,194 za mazao ya nafaka na tani 972,960 za mazao yasiyo ya nafaka,huku ukiwa na asilimia 120 hadi 240.

Wasindikaji wapewa mafunzo

Katika mradi huo pia watafanya kazi na wasindikaji kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, kwa kuwapatia mafunzo yanayohusiana na uzalishaji wa chakula kwa kufuata muongozo na matakwa ya sheria ya urutubishaji, vilevile viwango vya urutubishaji na usalama wa chakula.

“Hili suala linasimamiwa na serikali ombi langu kwa walimu hasa kwenye shule zilizolengwa wahakikishe wanatumia unga huo.

 Kwa kuwa wasipotumia wapo wataalamu watakaokuwa wanapita kwenye shule hizo kupima unga huo na wakibainika watachukuliwa hatua,” amesema Archard Ngemela,Meneja Urutubishaji chakula kutoka shirika la Global Alliance for Improved Nutrition (Gain).

Naye Afisa elimu jiji la Mwanza, Nyandaro Musagasa amewataka walimu kuhakikisha wanazingatia matakwa hayo kwa ajili ya kuwanusuru watoto dhidi ya matatizo ya udumavu.

“Watoto wanapokula vyakula vilivyorutubishwa wanakuwa katika ukuaji mzuri kiakili, kuzuia matatizo ya mgongo wazi, na wenye vicha vikubwa,” amesema Nyandaro.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV