Microsoft kuachilia Window 11 Oktoba

September 7, 2021 12:36 pm · Medlini
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni mfumo endeshi wa kompyuta utakaoingia sokoni mwezi ujao.
  • Utachukua nafasi ya Window 10.
  • Kompyuta mpya kuja na Window 11.

Dar es Salaam.  Kampuni ya teknolojia ya  Microsoft inatarajia kuingiza sokoni toleo jipya la mfumo endeshi wa kompyuta la Window 11 Oktoba 5 mwaka huu, ikiwa ni hatua ya kuboresha mifumo ya kifaa hicho cha kielektroniki.

Juni 24 mwaka huu, kampuni hiyo ya Marekani ilitambulisha toleo hilo na lilianza kutumika kwa majaribio na katika kipindi hicho imefanya masasisho saba kabla ya kufikia uamuzi wa kuruhusu watumiaji wake waanze kutumia mwezi ujao.

Mfumo huo mpya wa kompyuta unachukua nafasi ya Window 10 ambayo imedumu tangu mwaka. Hata hivyo, Window 10 itaendelea kuwepo sokoni tangu 2025 na inaweza kuwa upungufu wa baadhi ya vipengele. 

Microsoft imeeleza kuwa imefikia uamuzi wa kuiweka Window 11 sokoni kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi  ya watumiaji na  kompyuta, hivyo umuhimu wa kuwapatia mfumo endeshi ulio bora na unaokidhi mahitaji ya ni jambo lisilo epukika. 

Imesema kompyuta zote zitakazotengwa kwa sasa zitawekewa mfumo huo endeshi wa Window 11.

Mfumo endeshi wa kompyuta wa 11 unakuja na  muonekano wa kisasa na mpangilio mzuri  wa ikoni za programu zilizoonyeshwa katikati ya mwambao wa kazi, sauti mpya zimebuniwa kuwa za chini.

Pia inakuja na duka la programu na programu ya mpangilio ambayo ni rahisi kupanga programu nyingi kwenye skrini. 

Awali Microsoft ilisema itasaidia mfumo endeshi wa kompyuta 11 kufanya kazi kwa watengenezaji wa kompyuta na hivyo vifaa vyote ambavyo vinatimiza mahitaji ya mfumo huu vitapata masasisho ya bure katikati ya mwaka 2022.

Microsoft imesema utengenezaji wa mifumo endeshi ya kompyuta ambao ulioanza mwaka 1985 utabaki kuwa sehemu muhimu ya biashara ya kampuni hiyo kwa sababu asilimia 14 ya mapato yake yanayotoka mifumo hiyo.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW