Fahamu ukweli kuhusu matumizi ya vitakasa mikono

September 8, 2021 7:59 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Vitakasa mikono havichubui mikono kama vimethibitishwa.
  • Unaweza kutumia vitakasa mikono kwenye nchi zilizozuia pombe.
  • Vitakasa mikono vinapunguza kasi ya maambukizi ya Uviko-19.

Dar es Salaam. Vitakasa mikono almaarufu kwa Kiingereza “Hand Sanitizer” ni miongoni mwa afua dhidi ya maambukizi ya Corona (Uviko-19) endapo vitatumika kwa usahihi.

Ni njia rahisi ya kutakasa mikono endapo maji hayapatikani kwa urahisi hasa ukiwa sehemu yenye mkusanyiko wa watu ikiwemo usafiri wa umma.

Hata hivyo, matumizi ya afua hiyo yamezungukwa na sintofahamu mbalimbali kwa baadhi ya watu ikiwemo viungo vinavyotumika kutengeneza, kiasi cha kimiminika kinachohitajika kutakasa mikono na matumizi sahihi hasa kwenye maeneo ya umma.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa maelekezo muhimu kuhusu vitakasa mikono na namna sahihi ya kutumika. Hizi ni baadhi ya dondoo hizo:

Unaweza kutumia vitakasa mikono mara nyingi uwezavyo

Kati ya uzushi unaozunguka kwenye mitandao ya kijmii ni kuwa matumizi ya  vitakasa mikono mara kwa mara yanaweza kuwa na athari ikiwemo kubabuka mikono.

Kwa mujibu wa WHO, vitakasa mikono vilivyoidhinishwa na mamlaka za afya za kimataifa na za kitaifa, ni salama kwa matumizi na mtu anaweza kutumia mara nyingi awezavyo kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Corona lakini pia vimelea vingine.

Vitakasa mikono vyenye “alcohol” ni salama kwa yeyote kutumia

Matumizi ya “alcohol” (kiwango cha pombe) kwenye vitakasa mikono hayajadhihirisha hatari yeyote ya kiafya hadi sasa. Kwa mujibu wa WHO, alcohol inayotumika kwenye vitakasa mikono haina uwezo wa “kuchubua” rangi ya mkono wala vinyweleo.

Hata uwezo wa kusababisha mzio, WHO imeainisha kuwa kwa watu ambao unaweza kuwa na mzio wa viungo vya bidhaa za usafi, uwezekano wa mizio yao kuchochewa kwa kutumia vitakasa mikono ni mdogo.

Unataiwakutumia kitakasa mikono cha kutosha kupakaza kwenye mkono wako wote. Usibanie. Picha| Daily Maverick.

Vinaweza kutumika kwenye nchi zilizozuia pombe

Huenda baadhi wanahofia kutumia au kusafiri na vitakasa mikono vilivyotengenezwa kwa kutumia alcohol kwenda kwenye nchi ambazo pombe imepigwa marufuku.

Baadhi ya nchi hizo ni pamoja na Pakistan, Iran, India, Libya na sudan.

Hata hivyo, kutumia vitakasa mikono kwenye nchi hizi hakuwezi kukuacha matatani kwani vitakasa mikono hivi vimethibitishwa kufanya kazi za kiafya.

Kwa mujibu wa WHO, hata kitabu cha dini ya Kiislam, Quran kimeruhusu alcohol kutumika kwenye kutengeneza dawa.

“Bidhaa yoyote iliyotengenezwa kwa lengola kupunguza ugonjwa au kuchangia kwenye afya bora imeruhusiwa na Quran ikiwemo alcohol,” imesomeka kwenye tovuti ya WHO.

Kwenye maeneo yenye watu wengi, matumizi ya vitakasa mikono yatasaidia kukata mmyororo wa maambukizi. Picha| Brookings Institution.

Vitakasa mikono haviambukizi Corona

Kwa baadhi swali ni, kama ameshika hii chupa mtu ambaye ana Corona itakuwaje? Kwa mujibu wa WHO, kushika chupa ya kitakasa mikono wakati wa kuchukua kimiminika hicho, hakuwezi kukusababishia maambukizi kwani baada ya kujitakasa tu utakuwa umeondoa vimelea vyote.

Matumizi ya vitakasa kwenye sehemu zinazofikiwa na watu wengi ikiwemo maduka makubwa (super market) ni muhimu kwa ajili ya kukata mnyororo wa maambukizi.

“Kusafisha mikono ni njia kuu ya kuondoa uwezekano wa maambukizi,” inasema WHO.

Makala haya ni sehemu ya mfululizo ya ripoti maalum zinazoangazia namna ya kukabiliana na Uviko-19 nchini zinazofadhiliwa na Shirika la International Media Support (IMS) na Umoja wa Ulaya (EU).

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW