Fanya haya kuepuka msukumo wa makundi rika wakati wa Uviko-19

December 15, 2021 10:47 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kujiepusha na makundi sogozi yanayotuma habari za uzushi.

Dar es Salaam. Katika kipindi cha mlipuko wa ugonjwa wa Corona (Uviko-19), kila mtu ana jambo ambalo amelishikilia kama imani yake. Baadhi wameamua kupuuzia tahadhari ya ugonjwa huo huku wengine wakisita kupata chanjo.

Hayo hutokea kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa taarifa sahihi, msukumo hasi wa kundi fulani la watu na wakati mwingine ni matokeo ya habari za uzushi kuhusu ugonjwa huo.

Vijana huiita hali hiyo “kujazana ujinga”. 

Wakati inaweza kuwa jambo zuri kuwasikiliza washikaji zako, huenda ukawa unashindwa kusikiliza kitu kikubwa zaidi, nafsi yako.

Ni muhimu kufahamu kuwa rafiki yako asipopata chanjo na asipate maambukizi ya Uviko-19 haimaanishi kuwa na wewe utakuwa na bahati hiyo.

Hayo yote ni kwa sababu wewe na rafiki yako mnatofautiana mazingira, kipato, shughuli za kufanya mara baada ya kila mtu kurudi kwao.

Ili kuepuka msukumo wa makundi rika , inashauriwa kuwasikiliza zaidi wataalamu hasa linapokuja kwenye masuala ya afya yako. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi kupima afya, kuacha uoga

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi kupima afya, kuacha uoga

Nukta TV

Uwepo wa vifaa, madaktari uendane na huduma inayotakiwa

Uwepo wa vifaa, madaktari uendane na huduma inayotakiwa

Nukta TV

Rais Samia: Maradhi ya moyo, saratani kwa watoto yaongezeka Tanzania

Rais Samia: Maradhi ya moyo, saratani kwa watoto yaongezeka Tanzania

Nukta TV