Majaliwa: Tutawadhibiti wanyamapori, wananchi waishi kwa amani

June 9, 2022 12:19 pm · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya wanyamapori wakiwemo tembo kuvamia makazi ya watu
  • Mifumo kuimarishwa kuzuia wanyama hao kufanya uharibifu.
  • Vituo 32 vya kuhifadhia silaha kujengwa kando kando na hifadhi za wanyamapori.

Dar es Salaam. Huenda migogoro ya binadamu na wanyamapori ikapungua Tanzania, baada ya kuimarishwa kwa mifumo ya kuwadhibiti wanyama hao wasiingie kwenye makazi ya watu na kufanya uharibifu wa mali yakiwemo mashamba.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kuimarisha mifumo hiyo ambayo itazuia wanyamapori wakiwemo tembo kuingia katika makazi ya watu.

Majaliwa ameliambia Bunge jijini Dodoma leo (Juni 9, 2022) kuwa kutokana na juhudi za Serikali kuimarisha ulinzi na kuzuia uwindaji haramu wanyama wengi wameongezeka hivyo inaendelea kuwadhibiti wasiingie kwenye makazi ya watu.

 “Tutaimarisha ulinzi ili kuzuia wanyamapori kuingia kwenye makazi ya wananchi na kuhakikisha madhara hayo hayajitokezi tena. Tutaendelea kudhibiti maeneo hayo ili wananchi waishi kwa amani.” amesema Majaliwa.

Wizara ya Maliasili na Utalii inaratibu ujenzi wa vituo 32 vya kuhifadhia silaha kando kando ya maeneo yanayopakana na hifadhi za wanyamapori.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema lengo la Serikali ni kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori hao na kuwahakikishia wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni mwa usalama wao.

Majaliwa alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Mlalo Rashidi Shangazi aliyetaka kujua Serikali inafanya nini kuwalinda wananchi wanaoishi pembezoni mwa hifadhi wasiendelee kupata athari zinazosababishwa uvamizi wa wanyamapori

                                 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV