HESLB yazindua mfumo wa kidigitali wa kurejesha mikopo

June 11, 2022 10:29 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Utaondoa usumbufu kwa waajiri kupeleka marejesho ofisi za bodi hiyo.

Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imezindua rasmi mfumo wa kidigitali unaomwezesha mwajiri kuwasilisha makato na orodha ya wanufaika-wafanyakazi wake kwa njia ya mtandao kutoka popote alipo.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema mfumo huo ulianza kwa majaribio mwaka 2019/20 na sasa umekamilika na hivyo kuwawezesha waajiri na wanufaika kurejesha mkopo kwa urahisi.

“Zamani ilikuwa mwajiri inabidi atoke ofisini kwake aje HESLB kufanya malipo lakini kwa sasa anaweza kuwasilisha orodha ya wanufaika-wafanyakzi wake na makato kutoka popote alipo kwa kutumia mfumo wetu huu ambao anajiunga kupitia tovuti yetu (www.heslb.go.tz),” amesema Badru.

Kwa mujibu wa Badru, ambaye ameutangaza rasmi mfumo huo Juni 10, 2022) jijini Dodoma, mfumo huo pia unamwezesha mnufaika mmoja mmoja kupata taarifa za deni lake na utaratibu wa kurejesha kupitia tovuti ya HESLB.

“Kuanzia mwaka jana, imekusa ni rahisi sana, unaingia kwenye tovuti yetu, unabofya ‘rejesha mkopo’ au ‘repay loan’ na kufuata maelekezo ya kujisajili na utaendelea kupata taarifa ya deni lako palepale au hata kudai refund (makato yaliyozidi),” amesema Badru.

 Akizungumzia uzoefu wake katika kutumia mfumo huo, mwakilishi wa Shule ya Msingi Young Jai iliyopo Dodoma, Young Mi Cha ameshauri HESLB iboreshe mfumo kuwawezesha waajiri kuwatambua waajiriwa wapya kama walinufaika na mikopo ya elimu ya juu.

“Kuna wakati waajiriwa wapya wanadanganya, hivyo pamoja na uzuri wa mfumo huu, ninashauri uboreshwe ili mwajiri aweze kutambua mwajiriwa mpya kama ni mnufaika wa HESLB au hapana bila kumuuliza au kuleta jina kwenu kwa uhakiki kwanza,” amesema Young.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
8 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
8 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Ulinzi waimarishwa Dar, maduka yachelewa kufunguliwa

Ulinzi waimarishwa Dar, maduka yachelewa kufunguliwa

Nukta TV

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV