Rais Samia, Mkuu mpya wa Majeshi kuteta “inbox”

June 30, 2022 2:24 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Mkuu wa mpya wa Majeshi (CDF), Jacob Mkunda aapishwa Ikulu.
  • Rais Samia aahidi kumpa ushirikiano.
  • Jenerali Mabeyo kuteuliwa katika kazi nyingine.

Dar es Salaam. Rais Samia ameahidi kutoa ushirikiano kwa Mkuu wa mpya wa Majeshi (CDF), Jacob Mkunda na kuhusu maelekezo ya kikazi watazungumza “inbox”.

Jenerali Mkunda aliyeteuliwa jana anachukua nafasi ya Jenerali Venance Mabeyo ambaye amestaafu leo huku Rais Samia akiahidi kumteua katika nafasi nyingine kuendelea kulitumikia Taifa.

Rais Samia aliyekuwa akizungumza leo Juni 30, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akimuapisha Jenerali Mkunda amempongeza pamoja na viongozi wengine aliowateua huku akiwataka kuendeleza kazi nzuri aliyofanya Jenerali Mabeyo.

“Kwa wale niliowateua, nawapongeza na kuwatakia kazi njema, mkaanze pale Jenerali Mabeyo alipoishia. Najua kwenye Jeshi hakuna mtu kuingia na yake, ukifika unaanzia alipoachia mwenzio. Nawataka mkafanye kazi kama aliyetoka alivyofanya,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema kuhusu mambo mengine kwa aliwaowateua akiwemo Jenerali Mkunda “maelekezo zaidi tutazungumza inbox.”

Jenerali Mabeyo kupata kazi mpya

Rais Samia amesema Jenerali Mabeyo amestaafu akiwa kijana na bado ana nguvu na sifa za kuendelea kuteuliwa katika nyadhifa mbalimbali.

“Umemaliza utumishi wako ukiwa bado una nguvu hivyo nitaendelea kukuteua na kukupa majukumu uendelee kusaidia kulitumikia Taifa lako. Nadhani jioni ya leo tutakusikia kwenye bomba, Katibu Mkuu atakuwa amekwisha kupangia majukumu,” amesema Rais Samia.

Kiongozi huyo mkuu wa nchi amesema anamshukuru kwa kumjaalia Jenerali Mabeyo kumaliza utumishi wake akiwa bado ana nguvu na kwa kazi nzuri uliyoifanya katika utumishi wake kwani amefanya kazi yake kwa uadilifu mkubwa na umetumikia cheo chake kwa jitihada kubwa.

Kabla ya uteuzi huo, Jenerali Mkunda alikuwa Mkuu wa Tawi la Operesheni na Mafunzo katika Makao Makuu ya Jeshi.

Rais Samia jana pia alimpandisha cheo Meja Jenerali Salum Haji Othman kuwa Luteni Jenerali na alimteua kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo Meja Jenereali Othman alikuwa Kamishna wa Utafiti na Maendeleo Jeshini katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Pia alimteua Luteni Jenerali Mathew Edward Mkingule kuwa Balozi ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Wateule hao wote wameapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV