Viadudu milioni 9 kumaliza uharibifu zao la pamba Tanzania

August 6, 2022 6:45 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Vitasaidia kuua wadudu wanaharibu pamba.
  • Viadudu hivyo vimesambazwa katika mikoa 17.

Mwanza. Huenda wakulima wa pamba wakaongeza uzalishaji na tija kwenye kilimo baada ya wabunifu kuja na teknolojia ya kisasa inayoangamiza wadudu wanaoharibu zao hilo.

Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti wa Kilimo Ukiriguru Mkoani Mwanza wamekuja na suluhisho la kukabiliana na wadudu waharibifu baada ya kusambaza viadudu zaidi ya milioni 9 kwenye mikoa 17 inayolima zao la pamba.

Mikoa hiyo ni pamoja na Mwanza, Simiyu na Shinyanga.

Mkurugenzi wa Huduma za Usimamizi TCB), James Shimbe amesema uwepo wa wadudu hao unachangiwa na mabadiliko ya tabianchi hali inayosababisha uzalishaji wa zao hilo kuwa duni.

“Miaka ya nyuma aina hii ya wadudu hawakuwepo, ila kutokana na mabadiliko ya tabiaNCHI wameanza kuonekana kushambulia zao hilo hivyo kufanya uzalishaji kuwa mdogo,” amesema Shimbe.

Shimbe alikuwa akizungumza kwenye Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane kanda ya Magharibi yanayoendelea katika viwanja vya Nyamhongolo jijini Mwanza.

Amesema mbali na kupeleka viuwadudu hao kwa wakulima, lakini pia wanatumia mikakati mbalimbali kuhakikisha zao la pamba linazalishwa kwa tija.

Ametaja moja ya mikakati hiyo ni kutoa elimu kwa wakulima ya umuhimu wa kupanda miche kwa kufuata kanuni bora za kilimo.

Kwa sasa mkulima anatakiwa kupanda kwa sentimita 60/30 ambapo kwa shamba la hekari moja litakuwa na miche 44,444 kutoka miche 22, 222 iliyokuwa inapandwaa kwa sentimita 90/40 kwa shamba kama hilo.

“Pia kupitia balozi wa uhamasishaji wa zao la pamba , Agrey Mwanri anahamasisha wakulima wanafahamu matumizi sahihi ya unyunyizi wa viuatilifu, lakini pia kuhakikisha anapata kwa wakati viatilifu ili kuweza kupambana na wadudu waharibifu,” amesema Shimbe.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV