Mambo matano yatakayosaidia kukomesha uvuvi haramu Ziwa Victoria

September 10, 2022 6:50 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link

Wachuuzi wa dagaa wakichmbua dagaa  katika soko la mwaloni jijini Mwanza. Picha | Mariam John.


  • Kuanzisha mamlaka kamili ya ziwa hilo ili kuwa na uangalizi wa karibu.
  • Serikali kuongeza ushirikiano na wavuvi kwa kuwapatia zana za kisasa.
  • Kufanyika kwa doria za mara kwa mara.

Mwanza. Wadau wa sekta ya uvuvi wametoa mapendekezo mbalimbali yatakayosaidia kukomesha uvuvi haramu katika Ziwa Victoria ikiwemo kuongeza ulinzi wa ziwa hilo.

Uvuvi haramu umechangia kupungua kwa samaki katika ziwa hilo kutokana kuvuliwa kwa samaki wasio na sifa, jambo linaloathiri biashara ya bidhaa hiyo hasa katika Mkoa wa Mwanza.

Pia baadhi ya watu mkoani humo wanalalamikia kupanda kwa bei ya samaki ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Upendo Laiza ni mkazi wa jiji la Mwanza anasema kwa sasa bei za samaki hazishikiki si kwa mdogo au mkubwa. 

Samaki wa kawaida ambaye walikuwa wanamnunua kwa Sh3,000 hadi Sh5,000 miaka ya nyuma kwa sasa anauzwa kati ya Sh7,000 hadi Sh10,000.

“Hali ni ngumu samaki imebaki kuwa chakula cha matajiri kwa masikini kama sisi hatuwezi kununua bora tukanunue maharage siku ziende,” amesema Upendo.

Suluhu hii hapa

Chama cha Wavuvi Tanzania (Tafu) kimeiomba Serikali kutoa kibali cha Ziwa Victoria kuwa mamlaka kamili inayojitegemea ili iweze kudhibiti uvuvi haramu ambao umechangia samaki kupungua ndani ya ziwa hilo na kusababisha kitoweo hicho kupanda bei.

Akizungumza na Nukta Habari ofisini kwake, Mwenyekiti wa Tafu, Bakari Kadabi ameanisha mambo matano muhimu ambayo Serikali inatakiwa kuyafanyia kazi ili kulinda ziwa hilo kwa ajili ya kizazi kilichopo na kijacho.

Pendekezo la pili ni kuwa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ufugaji wa samaki na kununulia maboti zingine zitumike kwa ajili ya kulinda ziwa hilo kama wanavyofanya nchi jirani za Uganda.

“Kwa sasa Ziwa halina ulinzi na doria za mara kwa mara kama wenzetu wa Uganda ambao ziwa lao linalindwa na uvuvi haramu haupo kama huku, kifupi huku wameacha uhuru uliovuka mipaka,” amesema Kadabi.

Jambo jingine ambalo mwenyekiti huyo angependa kuona likifanyiwa kazi na Serikali ni kuunda kwa bodi ya pamoja itakayokuwa inashughulikia migogoro na changamoto za wavuvi.


Zinazohusiana:


Amesema kwa sasa hakuna kitengo ambacho kinashughulikia changamoto za wavuvi na kila sekta inaingia la kuleta hoja zake.

“Tukiwa na bodi itakuwa msimamizi mzuri wa sekta ya uvuvi ambayo pia itatumika pia kutoa mwelekeo wa bei za zao hilo kwa nje ya nchi kama wanavyofanya wenzetu wa sekta ya madini ambao hupata bei kabla ya kwenda kuuza mzigo wao,” amesema Kadabi.

Mwenyekiti huyo pia ameiomba Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia wavuvi ambao mwaka 2018 zana zao uvuvi ziliharibiwa vibaya kufuatia kampeni ya Operesheni Sangara.

Ameeleza kampeni hiyo haikulenga kutokomeza uvuvi haramu isipokuwa ililenga kuwafanya wavuvi kuwa masikini ambapo wavuvi walikufa na wengine kufilisiwa mali zao.

“Hadi sasa wavuvi wamefirisika na ndio maana fedha wanazopata wanakimbilia kununua zana za uvuvi za bei rahisi na wengine kuvua kwenye mazalia ya samaki,” amesema.

Katibu wa Tafu, Mayalu Zakayo amesema gharama nafuu ya umemejua (Solar) zinazotumika kwenye uvuvi huenda ikawa ni sababu mojawapo inayochangia uvuvi haramu.

Amesema wakati wavuvi wanatumia taa za kalabai kuvua uvuvi haramu ulikuwepo lakini haulingani na huu wa kutumia taa za umemejua.

“Mfano mvuvi analazimika kutumia taa zaidi ya moja kwenye mtumbwi na anaingia ziwani na betri la kuchaji pale taa zinapokaribia kuishiwa mwanga kitendo ambacho ni kinyume cha utaratibu wa matumizi ya taa hizo,” amesema Zakayo.

Ameitaka pia Serikali kutoa elimu kwa wavuvi kuhusiana na kukomesha uvuvi haramu huku akiwataka wavuvi wenyewe wajitambue na waache kutumia nguvu kuvua.

“Mpaka sasa hakuna sheria iliyotungwa kwa ajili ya kuzuia idadi ya umiliki wa mitumbwi kwa mvuvi, mfano mtu mmoja anamiliki mitumbwi ya kuvulia zaidi ya 100 na yote inaingia ziwani kuvua matokeo yake inavua na samaki ambao hawaruhusiwi,” amesema Zakayo

Ameiomba Serikali kuangalia namna ya kupunguza nguvu ya uvuvi na kuanzisha doria kali ziwani ili kunusuru ziwa hilo.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV