Madiwani Arusha, Ilemela wabadilishana uzoefu miradi ya maendeleo

January 17, 2023 12:41 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wakutana Mwanza kujifunza mkoa huo unavyotekeleza miradi ya kimkakati.

Mwanza. Timu ya madiwani na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imefanya ziara katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela yenye lengo la  kujifunza namna halmashauri hiyo ilivyoweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kutoa matokeo chanya.

Mradi mmojawapo ambao umevutia na kuwa chao ya wao kutembelea ni stendi ya mabasi na maegesho ya malori uliopo Nyamh’ongolo mkoani Mwanza.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi huo uliogharimu zaidi ya Sh26 bilioni zikiwemo gharama za maegesho ya malori na gharama za mshauri, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Ojung’u Salekwa amepongeza juhudi zilizofanywa na timu ya Ilemela kuhakikisha wanakamilisha kazi hiyo ya ujenzi wa stendi ya kisasa.

“Kwa hiki kinachoonekana ni dhahiri kuwa Ilemela kuna ushirikiano mzuri kati ya madiwani na wataalam, tumefurahishwa na kazi iliyofanyika hapa na tutaiga mfano wenu,” amesema Salekwa.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulinga amepongeza uamuzi wa madiwani na wataalam hao kutembelea Ilemela kwa ajili ya kujifunza na kuelezaa kuwa hilo ni jambo la kutia moyo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Apolinary, amesema kazi ya ujenzi wa stendi hiyo imefanywa kwa ushirikiano mkubwa wa madiwani na wataalamu wa halmashauri hiyo.

“Tuna kauli mbiu yetu kuwa Ilemela ni yetu sote tushirikiane kuijenga hivyo kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kuwajibika kuhakikisha tunakamilisha miradi yote tuliyojiwekea,” amesema Apolinary.

Amesema kwa sasa halmashauri hiyo imeendelea kuibua vyanzo mbalimbali vya mapato pamoja na kuboresha usimamizi wa vilivyopo.

Mtaalam wa miradi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela James Wembe, amesema ni vizuri kushirikisha wataalam washauri wa ndani na nje ya halmashauri kutoa mawazo yao katika masuala ya miradi inayotekelezwa eneo husika.

“Zipo hatua za kufuata katika kufanikisha miradi mikubwa kama hii, kuanzia mpango (planning), utekelezaji (Implementations) na kazi yenyewe (operations),” amesema Wembe.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV