15 washikiliwa, msako wenye magari namba SSH 2530

September 4, 2025 6:27 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Muliro asisitiza kuwa kutumia namba hizo ni kosa kisheria

Dar es salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za kuendesha magari yenye namba SSH 2530, kinyume na sheria. Hatua hiyo ni mwendelezo wa operesheni ya kuhakikisha maagizo yaliyotolewa awali kuhusu marufuku ya namba hizo yanatekelezwa ipasavyo.

Akizungumza leo Alhamisi, Septemba 4, 2025, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema watuhumiwa tayari wamekamatwa huku msako dhidi ya wengine ukiendelea.

“Mtu yeyote anayebandika namba hizo, baada ya kufuatiliwa kwenye mifumo ya usajili wa namba, hili ni kosa kisheria,” amesema Muliro.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, amesema watuhumiwa tayari wamekamatwa huku msako dhidi ya wengine ukiendelea. Picha | Mwananchi.

Kwa mujibu wa Muliro, watu hao wamekamatwa kwa mujibu wa Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 Marejeo ya 1973 yaliyorekebishwa mwaka 2023, ambayo inaeleza kuwa ni kosa la jinai kwa mtu yeyote kuendesha chombo cha moto bila namba halali za usajili na yeyote anayekiuka hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

“Tunaendelea kusisitiza kuwa ni makosa na suala hili ni kinyume cha sheria kwa sababu namba hizo hazipo,” amesisitiza Muliro.

Itakumbukwa kuwa Agosti mwaka huu, Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Msemaji wake, David Misime, lilitangaza marufuku ya matumizi ya namba hizo na kuwataka wamiliki wa magari kuondoa ifikapo Septemba 1, 2025. 

Kutoka kwa marufuku ya Jeshi la Polisi kumekuja hiyo mara baada ya vyombo mbalimbali vya moto kuonekana vikitumia namba hiyo hivi karibuni jambo lililozua mijadala hususan katika majukwa mbalimbali ya mitandao ya kijamiii huku wengine wakihusisha utumiaji wa namba hizo na siasa katika kipindi kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV