Zingatia haya kuwa na afya bora ya akili
- Ni pamoja na kupata muda mzuri wa kupumzika, kufanya mazoezi na kuzungumza.
- Inashauriwa pia kujifunza njia za ukabiliana na msongo wa mawazo
Dar es Salaam. Wakati watu wanawekeza katika afya ya mwili kwa kula chakula bora, kufanya mazoezi na kujiepusha na baadhi ya tabia hatarishi kwa afya, baadhi yao husahau afya ya akili.
Kutokujali afya ya akili kumewafanya kuingia katika changamoto za maisha ambazo imekua vigumu kuzitatua.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), afya ya akili ni hali ya mtu binafsi kuwa na uwezo na kukabiliana na changamoto za kimaisha, kutambua nguvu ambazo anazo na kufanya maamuzi sahihi.
Hata hivyo, zipo baadhi ya tabia ambazo zinamfanya mtu kushindwa kufanya kazi kwa ustadi na kusahau nguvu (ability) yake na hivyo kuathiri uwezo wake wa kupambana na changamoto na kujikuta akiwa katika msongo wa mawazo.
Tabia hizo ni pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya, matumizi ya pombe na kushindwa kutatua changamoto za kimaisha mapema.
Ni tabia zipi ambazo unashauriwa kuachana nazo ili kuwa na afya njema ya kiakili? tazama video hii kujifunza zaidi.
Latest