Zanzibar kama Bara: Kufungua vyuo, kidato cha sita Juni mosi

May 27, 2020 8:35 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Vyuo vote vitafunguliwa Juni mosi  na kuruhusu ligi kuu ya mpira wa miguu ianze tena. 
  • Pia wanafunzi wa kidato cha sita kurejea shuleni siku hiyo hiyo.
  • Wananchi watakiwa kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na Corona. 

Dar es Salaam. Hatimaye Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imechukua uamuzi unaofanana na Tanzania wa kufungua vyuo vyote Juni 1 mwaka huu sambamba na kuruhusu ligi kuu ya mpira wa miguu ianze tena. 

SMZ pia imeruhusu wanafunzi wa kidato cha sita kurejea shuleni Juni mosi kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ya kuhitimu kidato hicho.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema baada ya Serikali kukabiliana kwa kiasi kikubwa na mlipuko wa Corona (COVID-19) inachukua uamuzi wa kulegeza baadhi ya masharti yaliyokuwa yameamuliwa hapo awali ikiwemo kufungua vyote ifikapo Juni mosi. 

“Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kuhakikisha kuwa kuanzia Juni 1, 2020 vyuo vyote vya elimu ya juu vitafunguliwa na kuendelea na programu zao kama kawaida,”

“Wanafunzi wa kidato cha sita nao wataanza masomo yao Juni 1, 2020 ili kuwezesha kufanya mitihani yao ya Taifa,” amesema Balozi Iddi.  

Kufuatia maamuzi hayo, ameagiza Wizara ya Mafunzo na Amari kushirikiana kikamilifu na Wizara ya afya katika kuandaa miongozo ya kiafya itakayopaswa kuzingatiwa ili kuepuka maambukizi ya maradhi haya kwa wanafunzi.

Aidha, wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha tano pamoja na wanafunzi wa shule za msingi, madrasa na vyuo vyao vitaendelea kufungwa hadi itakapotolewa maelekezo mengine ya Serikali hapo baadaye. 


Zinazohusiana


Kuhusu michezo, Balozi Iddi amesema Ligi kuu ya mpira wa miguu Zanzibar itaendelea kuanzia Juni 5, 2020 na ameiagiza Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Chama Cha Soka Zanzibar (ZFF) na Wizara ya Afya kuandaa mwongozo wa kuendesha ligi hiyo.

“Kwa upande wa michezo mingine ya vilabu au makundi ya wananchi na mtu mmoja mmoja ikiwemo mazoezi, mashindano ya uwanjani au ufukweni yote yatasubiri hadi itakapotolewa taarifa nyingine hapo baadaye,” amesema makamu huyo wa Rais Zanzibar. 

Tangu ugonjwa wa virusi vya Corona uliporipotiwa kwa mara ya kwanza Machi 18 hadi sasa viwani humo, amesema wagonjwa 134 wamethibitishwa kuwa na maradhi hayo huku sita wakifariki dunia.

Kati yao wagonjwa 109 wamepatikana Unguja na waliobaki wanatoka Pemba. 

“Jumla ya wagonjwa 115 wamepona na wagonjwa 19 tu ndiyo wanaondelea na matibabu katika kambi za matibabu za Unguja na Pemba,” amesema Balozi Iddi.

SMZ imewataka wananchi wa visiwa hivyo kuendelea kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya ikiwemo kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa huo. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV