Yafahamu maziwa makubwa matano Tanzania

September 13, 2019 5:22 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Maziwa ya Eyasi, Rukwa, Nyasa, Tanganyika na Victoria ndiyo maziwa makubwa zaidi nchini Tanzania.
  • Yanatumika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kuwanufaisha wananchi na Taifa ikiwemo uvuvi na utalii.

Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa rasimili nyingi za asili ambazo zimekuwa zikitumiwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kuwanufaisha wananchi na Taifa ikiwemo uvuvi na utalii.

Rasimali hizo ni mito, milima, maziwa, wanyama, madini. Kuzitaja ni chache. Endapo ulikua hufahamu maziwa makubwa matano zaidi nchini Tanzania, www.nukta.co.tz ipo kwa ajili ya kukufahamisha maziwa hayo na maeneo yalipo nchini. 

Uchambuzi wa Takwimu muhimu (Tanzania in figures 2018) zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha maziwa ya Eyasi, Rukwa, Nyasa, Tanganyika na Victoria ndiyo maziwa makubwa zaidi nchini. 

5. Ziwa Eyasi

Ziwa la Eyasi ni ziwa la tano lenye kina kirefu Tanzania bara lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1, linapatikana askazini mwa Tanzania na nyanda za juu kaskazini mashariki mwa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. 

Shughuli mbalimbali kama utalii na uwindaji wa wanyama zimekuwa zikifanyika katika ziwa hilo. Kitu cha kipekee kilichopo katika ziwa hilo ni maji yake huongezeka na kupungua kulingana na nyakati mbalimbali za mvua katika eneo hilo.

4. Ziwa Rukwa

Ni ziwa la nne lenye ukubwa kilomita za mraba 2.8, linafahamika kwa mamba wengi pamoja na ndege wa aina tofauti. Ziwa hili halina chanzo kinachoingiza maji bali hutegemea zaidi mvua.

Inapatikana Kusini Magharibi mwa Tanzania, karibu na nchi ya Zambia. Pia liko katikati ya ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa. Ziwa Rukwa ni ziwa kubwa la magadi nchini Tanzania, ambalo pia liko kwenye mkondo wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

3. Ziwa  Nyasa 

Ziwa Nyasa ni ziwa la tatu kwa ukubwa Tanzania kwa kilomita za mraba 5.6 likiwa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania. Kusini mwa ziwa unatoka Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.

Kijiolojia ziwa hilo ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. Ziwa Nyasa linajulikana kuwa na aina nyingi za samaki (zaidi ya 1500) huku aina chache tu zinavuliwa kama chakula, lakini aina mbalimbali zinakamatwa na kuuzwa nje ya Afrika kwa wapenzi wa samaki wa rangi.


Zinazohusiana: 


2. Ziwa Tanganyika

Hili ni ziwa la pili kubwa Tanzania na duniani lenye sifa ya maji mengi. Maji yake hutoka kuelekea mto Kongo na hatimaye katika Bahari ya Atlantiki. 

Ziwa hilo ambalo linategemewa zaidi na wakazi wa Tanzania kwa uvuvi na kilimo lina kilomita za mraba 13.4 na likipambwa na visiwa mbalimbali ambavyo vimekuwa vikitumiwa kwa shughuli za utalii.

Ziwa Tanganyika lina Hifadhi mbili za Taifa katika fukwe zake za Gombe na Mahale ambazo ndizo Hifadhi pekee nchini Tanzania wanakopatikana wanyama aina ya Sokwemtu (Chimpanzee) wanaoishi katika mazingira yao ya asili milimani.

Lakini limekuwa kiungo muhimu na nchi za jirani za Mawaziwa makuu ikiwemo Burundi. 

Mto mkubwa zaidi unaoingia ni Ruzizi unaofika upande wa kaskazini kutoka Ziwa Kivu. Malagarasi, ambao ni mto mrefu wa pili nchini Tanzania, inaingia upande wa mashariki. Picha|Mtandao.

 1. Ziwa Victoria 

Ziwa victoria ni ziwa la kwanza kwa ukubwa hapa Tanzania lenye kilomita za mraba 34.9 lililopo baina ya Tanzania, Kenya na Uganda. 

Ziwa hili linapata maji yake kwa mvua pamoja na vijito vyake. Jina la ziwa hili lilitokana na jina la aliyekua Malkia wa Uingereza. 

 Ziwa Victoria lina samaki aina ya 400, na baadhi yao hawapatikani mahali pengine ulimwenguni. Wanaopatikana zaidi ni perege na ngege.

Enable Notifications OK No thanks