Windlab, Eurus kuongeza nguvu uzalishaji umeme wa upepo Tanzania

March 6, 2019 10:24 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Kampuni hizo zitaweza Sh23 bilioni kuendeleza mradi wa uzalishaji wa umeme wa upepo wa katika nchi za Afrika ukiwemo wa ‘Miombo Hewani’ mkoani Njombe na kuwapunguzia wananchi adha ya umeme. 
  • Uwekezaji huo pia utagusa nchi za Ethiopia, Kenya, Tanzania, Zambia, Uganda, Rwanda, Burundi na Malawi. 
  • Tanzania ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,600 za umeme na inatarajia kuongeza uzalishaji wa megawati 2,100 itakapokamilisha ujenzi wa mradi wa Stiegler’s Gorge.

Dar es Salaam. Huenda watanzania wakaondokana na tatizo la uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme katika maeneo yao, kutokana na kampuni za kimataifa kuongeza nguvu katika utekelezaji wa mradi wa uzalishaji wa umeme wa upepo katika mkoa wa Njombe. 

Kampuni za Windlab Limited (WND) ya nchini Australia na Eurus Energy Holdings Corporation (Eurus) ya Japan wameamua kuwekeza mtaji wa Dola za Marekani 10 milioni (Sh23 bilioni) katika kampuni ya Windlab Africa Pty Ltd (WA) ili kuimarisha utendaji na uendelezaji wa miradi ya uzalishaji umeme wa upepo katika nchi za Afrika.

Kampuni hiyo ya WA yenye makao makuu nchini Afrika Kusini inakusudia kutekeleza miradi ya uzalishaji umeme wa upepo katika nchi za Ethiopia, Kenya, Tanzania, Zambia, Uganda, Rwanda, Burundi na Malawi ambapo Mei, 2018  ilipata cheti cha tathmini ya mazingira na athari za kijamii (ESIA) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa uzalishaji wa umeme wa upepo wa Megawati 300 katika shamba la ‘Miombo Hewani Wind’ lililopo mji wa Makambako mkoani Njombe. 

Taarifa iliyotolewa na kampuni ya WND imeeleza kuwa uwekezaji huo utasaidia kukamilisha uundaji wa mfumo wa kisheria kuendesha kampuni ya WA ambapo kukamilika kwake kutaiwezesha Eurus kumiliki hisa kwa asilimia 25. 

“Rasilimali za WA kwa sasa zinajumuisha miradi 16 ya maendeleo ambayo inatarajia kuzalisha megawati 1,650 za umeme wa upepo, kutoka katika hatua za awali hadi mradi wa megawati 300 wa shamba la Miombo Hewani nchini Tanzania ambao umepitishwa na serikali ya nchi hiyo,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo. 


Kufahamu zaidi:


Ujio wa Eurus katika kampuni ya WA utaiwezesha pia kuwa na wawakilishi katika Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo na kuongeza kasi ya ujenzi wa miradi katika nchi tajwa.

Taarifa hiyo inaeleza zaidi kuwa WA itatumia fedha hizo pia kuendeleza miradi yake katika nchi za Afrika Mashariki ili kuyafikia maeneo mengi ambayo yanahitaji umeme. 

Benki ya Dunia (WB) inakadiria kuwa idadi ya watu katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara imevuka bilioni moja ambapo baadhi ya nchi uchumi wake unakuwa kwa kasi ikiwemo Ethiopia kwa asilimia 8.2, Kenya (5.5%) na Tanzania (6.8%).

Licha ya ukuaji huo wa uchumi, upatikanaji na uwezo wa uzalishaji umeme ni wa kiwango cha chini. Mathalani Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 59 milioni lakini ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,600 za umeme ukilinganisha na Australia inayozalisha megawati 50,000. 

“Umeme wa upepo na jua ni vyanzo rahisi na teknolojia inayokua haraka kama itatumiwa vizuri itasaidia kukidhi mahitaji ya upatikanaji wa nishati jadidifu na mabadiliko ya utendaji wa WA yatajikita zaidi kuwekeza katika fursa hizo,” ameeleza Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Windalab, Roger Price katika taarifa hiyo iliyotolewa Februari 26, 2019.

Uzalishaji wa umeme wa upepo nchini utasaidia kupunguza adha ya umeme katika maeneo mmbalimbali. Picha|Mtandao.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Eurus, Hideyuki Inazumi amesema ubia huo waliongia na WA utasaidia kuibua na kuendeleza rasilimali za upepo katika soko la nishati jadidifu katika nchi za Afrika zenye mahitaji makubwa ya nishati.

Mradi wa Miombo Hewani utatekelezwa kwa awamu mbalimbali ambapo katika hatua za awali  utazalisha megawati 100 kwa kutumia mashine 34 zitakazofungwa katika shamba hilo  na kuunganishwa katika mfumo wa umeme katika kituo kidogo cha gridi ya umeme ya  Taifa cha Makambako.

Kukamilika na kuanza kufanya kazi kwa mradi huo kunatarajia kuwafikia watu 3 milioni kwa nishati ya umeme wa upepo, jambo litakalosaidia kupungua kero ya kukatika kwa umeme nchini.

Habari hii imeboreshwa kwa kubadili kiwango cha uwekezaji kilichofanywa na kampuni ya za Windlab Limited (WND) ya nchini Australia na Eurus Energy Holdings Corporation (Eurus) ya Japan.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
14 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
14 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV