Wiki yaisha kwa machungu Soko la Hisa Dar

February 29, 2020 10:24 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Thamani ya mauzo ya wiki nzima imeshuka kwa takriban asilimia tatu hadi Sh18.7 bilioni kutoka Sh19.3 milioni iliyorekodiwa juma lililopita.
  • Wachambuzi waeleza kuwa licha kushuka kwa thamani ya mauzo, matumaini ya kufanya vizuri katika soko hilo bado yapo.

Dar es Salaam. Thamani ya mauzo ya wiki nzima katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) imeshuka kidogo kwa takriban asilimia tatu hadi Sh18.7 bilioni kutoka Sh19.3 milioni iliyorekodiwa juma lililopita huku wachambuzi wakitabiri mwenendo chanya siku zijazo.

Uchambuzi wa soko kwa wiki iliyoanzia Februari 21 hadi 28, 2020 uliofanywa na kampuni ya udalali ya masoko ya mitaji na dhamana, Zan Securities, unabainisha kuwa thamani ya mauzo katika soko hilo ulishuka  kwa asilimia 2.6 kutoka yale ya wiki iliyopita.

Wiki za DSE hujumuisha siku za kazi pekee yaani Jumatatu hadi Ijumaa.


Soma zaidi: Thamani ya mauzo soko la hisa Dar yapaa zaidi ya mara 40


“Licha ya kushuka thamani ya mauzo, bado soko linatoa matumaini ya kufanya vizuri siku zijazo kwa sababu kiasi na mauzo ya jumla ya wiki yako  thabiti katika viwango vya mabilioni,” imesema taarifa iliyotolewa leo (Februari 29, 2020) na Mtendaji Mkuu wa Zan Securities, Raphael Masumbuko.

Wakati thamani ya mauzo ya jumla ya DSE ikishuka, benki ya NMB imechangia asilimia 94 ya thamani mauzo yote ya wiki iliyoishia Februari 28.

NMB imefuatiwa kwa mbali na kampuni ya bia Tanzania (TBL) ambayo imechangia asilimia 2.9 na benki ya CRDB kwa asilimia 2.85.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV