Watumiaji X (Twitter) sasa kufahamika walipo

November 27, 2025 5:01 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kipengele ambacho kinaweka wazi taarifa muhimu kuhusu asili na mwenendo wa akaunti pamoja na mahali ambapo akaunti ilifunguliwa.

Dar es Salaam. Mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) umeweka kipengele kipya kinachoweka wazi taarifa muhimu kuhusu ikiwepo mahali alipo mtumiaji wa akaunti hiyo, majina yaliyobadilishwa pamoja na mwaka ambao akaunti ilifunguliwa.

Maboresho hayo yanalenga kudhibiti matumizi ya akaunti feki pamoja na kusambaa kwa taarifa potofu, 

Kwa mujibu wa Mkuu wa Bidhaa wa X, Nikita Bier, hatua hiyo inalenga kuongeza uwazi na kuwapa watumiaji muktadha wa kutosha ili kutambua uhalisia wa akaunti.

Kipengele hicho kipya, kinaitwa ‘About this Account,’ ambacho kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye mashirika ya habari ya The New York Times na BBC, kitaonyesha nchi ambako akaunti ilifunguliwa, mara ngapi mtumiaji amebadili jina la akaunti, pamoja na aina ya mfumo anaotumia kuendesha akaunti hiyo kama ni Android au iPhone.

Aidha, mtumiaji wa mtandao wa X anaweza kuangalia taarifa za “About this Account”  juu ya ukurasa wa wasifu wa mtumiaji anapoingia katika akaunti yake ya mtandao huo.

Mtumiaji atakapoingia katika ukurasa huo atatakiwa kubofya sehemu iliyoandikwa ‘Joined’ ambayo iko chini ya jina lake, aidha atakapofanya hivyo atapelekwa moja kwa moja kwenye ukurasa maalum unaoonyesha maelezo yanayohusu akaunti yake kwa kina.

Mtandao wa X ulianzishwa mwaka 2006 na Jack Dorsey, Evan Williams, Biz Stone na Noah Glass, kwa jina la awali ‘twttr’ kabla ya kubadilishwa kuwa Twitter. 

Twitter ilibadilishwa jina na kuwa X Julai 2023 mara baada ya kununuliwa na Bilionea Elon Musk mnamo Oktoba 27, 2022 kwa kiasi cha Dola 44 bilioni za Marekani sawa na Sh108 trilioni.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Oct, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

BoT yauza tani 5 za dhahabu kuongeza fedha za kigeni

Nukta TV