Wanahabari wa Tanzania, Kenya kukutana jukwaa moja la tabianchi Ghana

February 14, 2019 10:02 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Wewe ni Mwanahabari unapenda kufaidika na fursa za mafunzo ya kuendeleza taaluma yako? Shirikia lisilokuwa la Kiserikali la Hivos litawakutanisha Wanahabari kutoka nchi za Kenya na Tanzania, katika kipindi cha wiki moja kuwajengea uwezo katika masuala ya tabianchi na mazingira. 

Muda huo utahusisha siku moja ya mafunzo; uwezekano wa kutembelea mradi mdogo wa kuzalisha umeme na siku tatu za kuhudhuria Mkutano wa Wiki ya Tabianchi Afrika (Africa Climate Week) utakaofanyika kati ya Machi 18-22, 2019 Jijini Accra, Ghana.na kuwahusisha wadau mbalimbali wa sekta ya umma na binafsi. 

Washiriki wa mkutano huo watajikita zaidi kuibua mbinu zitakazosaidia ushirikiano baina ya wadau katika sekta mahususi kama nishati, kilimo na maendeleo ya makazi.

Mwanahabari wa aina gani unayehitajika?

  • Umewahi kupata mafunzo na Hivos na umezalisha habari kuhusu nishati jadidifu baada ya mafunzo.
  • Unapenda sana kuripoti masuala ya nishati jadidifu ama mabadiliko ya tabianchi.
  • Utakuwa tayari kutengeneza mpango wa uzalishaji habari kabla ya mkutano na kuzalisha habari wakati na baada ya mkutano.

Kama ni miongoni mwa Wanahabari wenye sifa hizo basi hiyo ni fursa muhimu kwako. Kufahamu zaidi jinsi ya kutuma maombi na maelezo muhimu soma zaidi hapa.  

Enable Notifications OK No thanks