Wafanyabiashara wadogo kujumuishwa ukusanyaji wa maoni Mkumbi II

June 6, 2025 7:26 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Serikali ya Tanzania imesema ili kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo nchini itawashirikisha katika utayarishaji wa  Mpango wa Pili wa Maboresho ya Mazingira ya Biashara na Uwekezaji (MKUMBI II).

Mkumbi ni mpango wa Serikali  unaolenga kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuvutia uwekezaji kwa kupunguza vikwazo vya kiutaratibu, kuboresha mifumo ya kisera, na kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi kustawi.

Lengo kuu la Mkumbi ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa mahali rafiki kwa wafanyabiashara wa viwango vyote ikiwemo wafanyabiashara wadogo, wakubwa na wakati na kuwa kivutio kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa.

Lengo kuu la Mkumbi ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa mahali rafiki kwa wafanyabiashara wa viwango vyote na kuwa kivutio kwa wawekezaji wa ndani na wa kimataifa. Picha | Global Publishers.

Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Juni 6, 2025, amesema Serikali imechukua uamuzi huo naada ya kubaini  malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu mazingira ya uendeshaji biashara, licha ya kazi kubwa iliyofanyika chini ya MKUMBI I.

Prof Mkumbo amesema Serikali iko tayari kupokea maoni na kuyatumia kuboresha zaidi katika mpango wa pili ambapo tayari kamati ya mpango huo imeshafanya uchambuzi wa mpango wa awali uliokuwa unatekelezwa tangu mwaka 2018.

Kwa sasa kamati hiyo kwa mujibu wa Prof Mkumbo inaingia katika hatua ya ukusanyaji wa maoni kutoka kwa wafanyabiashara na wawekezaji ikiwalenga zaidi wafanyabiashara wadogo na wa kati ikiwemo wafanyabiashara wa chakula maarufu kama mama lishe. 

“Tunakwenda kuonana na wadau wa biashara na uwekezaji kwenda kuzungumza nao kupata maoni yao, kupata mapendekezo yao kujua ni mambo yapi tunapaswa kuyazingatia ili biashara zilendelee kukua” ameeleza Profesa Mkumbi.

Aidha, kwa upande wake mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Faustine Kabuzora amesema kuwa mchakato huo unatarajiwa kuanza mnamo Juni 16, 2025 ukijumuisha mikoa 16. 

Ukusanyaji wa maoni utaanzia katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro pamoja na Dodoma kisha kuelekezwa katika mikoa mingine.

“Biashara ndogondogo zinajumuisha watu wengi sana, kwaiyo na wenyewe tutawajumuisha kuwauliza ni jinsi gani wanadhani mazingira yao ya biashara yaboreshwe,” amesema Profesa Kabuzora.

Ushirikiswaji wa wafanyabiashara wadogo kwenye mpango huo unaweza kusaidia kutatua kero zao na uboreshwaji wa mazingira yao ya biashara kama kuwepo sera rafiki zinazolenga kupunguza urasimu, gharama zisizo za lazima, na kero zinazokwamisha biashara zao. 

Pia, hatua hii inaweza kuchochea uanzishwaji wa huduma bora zaidi kama vile miundombinu ya masoko, maeneo rasmi ya kufanyia biashara, mikopo yenye masharti nafuu na mafunzo ya ujasiriamali. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV