Wafanyabiashara kuwekewa kitengo huru ‘kuisuta’ TRA

June 13, 2019 2:29 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Kitengo hicho kitawawezesha kutoa malalamiko ya mbalimbali ya kodi ikiwemo rushwa na makadirio yasiyoendana na biashara. 
  • Kitaratibiwa na Wizara ya Fedha na Mipango ili kuondoa malalamiko ya muda mrefu. 

Dar es Salaam. Huenda wafanyabiashara nchi wakapata ahueni ya kupunguziwa kero za kodi, baada ya Serikali kupendekeza kuanzisha kitengo huru cha kupokea malalamiko ya taarifa za kodi dhidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango aliyekuwa akizungumza bungeni leo (Juni 13, 2019) wakati akiwasilisha bajeti ya Serikali Kuu kwa mwaka 2019/2020, amesema kitengo hicho kitasimamiwa na kuratibiwa na wizara yake ili kuhakikisha kinakuwa na ufanisi wa kushughulikia kero za wafanyabiashara.

“Kitengo hiki kitahusisha kupokea na kupitia malalamiko ya kodi zinazotolewa na walipa kodi au watu wenye nia njema,” amesema Dk Mpango.  

Ameweka wazi baadhi ya majukumu ya kitengo hicho ikiwemo kupokea malalamiko ya rushwa dhidi ya watumishi wa TRA ambao wamekuwa wakijipatia fedha kinyume na sheria na kuwakandamiza wafanyabiashara. 


Zinahusiana: 


Aidha, kitengo hicho kitapokea malalamiko ya ukadiriaji wa kodi na uthaminishaji wa bidhaa husika pasipo kufuata taratibu zilizowekwa na malalamiko ya matumizi ya nguvu katika ukusanyaji wa kodi dhidi ya TRA.

Lakini kitengo hicho kitapokea malalamiko ya ufungaji biashara bila kufuata sheria, taratibu za TRA na kero zozote zinazohusiana na kodi dhidi ya mamlaka hiyo kodi nchini.  

Huenda kitengo hicho kitasaidia kupunguza kero za muda mrefu za kodi ambazo zimekuwa kikwazo katika ukuaji wa shughuli za biashara nchini.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW