Wafanyabiashara Kariakoo watii maagizo wahama barabarani

February 17, 2026 11:22 am · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Wafanyabiashara wa ndani ya soko wasema uwepo wa wafanyabiashara wanomwaga bidhaa nje ya soko unafanya wateja wengi kuishia nje jambo linalowakosesha mapato na wateja.

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa soko la kimataifa la Kariakoo wametii maagizo yaliyotolewa na viongozi mbalimbali wa serikali yaliyowataka kuacha kufanya biashara maeneo yasiyoidhinishwa ikiwemo barabarani.

Nukta Habari ilipita katika baadhi ya mitaa inayozunguka soko hilo ambayo awali ilikuwa imezongwa na wafanyabiashara hao na kujionea barabara zikiwa tupu bila misongongamano hiyo.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku nane tangu soko hilo lizunduliwe na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Februari 8, 2026 baada ya takribani miaka mitano tangu soko hilo liteketee kwa moto Julai 10, 2021. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara wa ndani ya soko hilo wanasema kuwepo kwa wafanyabiashara wanomwaga bidhaa nje ya soko kunafanya wateja wengi kuishia nje jambo linalowakosesha mapato na wateja.

Katibu Msaidizi na kiongozi wa sakafu ya ardhini ‘Ground Floor” wa soko hilo Thomas Philipo ameiambia Nukta Habari kuwa kuwepo wa wafanyabiashara wanaopanga bidhaa nje ya soko kunachangia wanunuzi wa bidhaa kuishia nje na hivyo kulikosesha soko na wafanyabiashara ambao wanalipa kodi kwa Serikali mapato. 

Hata hivyo, licha kuonekana wafanyabiashara hao wametii maagizo ya viongozi Nukta Habari imeshuhudia Jeshi la Polisi likifanya doria wakati wote kuzunguka soko hilo ambapo kwa mujibu wa Philipo doria hiyo ni kwa ajili ya kukamata yeyote atakayepanga bidhaa katika maeneo yasiyoruhusiwa ukiachilia mbali ulinzi na usalama wa soko.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wakazi wa mabondeni Dar walivyojiandaa kukabiliana na ‘El Nino’

Wakazi wa mabondeni Dar walivyojiandaa kukabiliana na ‘El Nino’

Nukta TV

Wakazi Kigogo wahofia ‘El Niño’, walia mchepuo wa daraja uondolewe

Wakazi Kigogo wahofia ‘El Niño’, walia mchepuo wa daraja uondolewe

Nukta TV

Ufahamu 'BIPOLAR' Part 2 | Ugonjwa wa afya ya akili unaoweza kupelekea kifo

Ufahamu 'BIPOLAR' Part 2 | Ugonjwa wa afya ya akili unaoweza kupelekea kifo

Nukta TV