Vyakula vya kuepuka kujilinda na ugonjwa ya figo

March 18, 2026 9:09 am · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na vyakula vyenye kiasi kikubwa cha protini, chumvi na kalsiamu.

Dar es Salaam. Ugonjwa wa figo ni miongoni mwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayozidi kuongezeka duniani, yakichangia vifo vya mamilioni ya watu duniani kote.

Takwimu zinaonesha asilimia saba ya Watanzania wanaugua ugonjwa sugu wa figo, ukiwathiri zaidi wakazi wa mjini kwa asilimia 15 kulinganisha na asilimia mbili za wakazi wa vijijini.

Awali ugonjwa huu uliripotiwa zaidi kwa wazee wenye umri wa zaidi miaka 45, lakini miaka ya hivi karibuni maradhi hayo yamekuwa yakishambulia watu wa rika zote ikichangiwa zaidi na mtindo mbovu wa maisha.

Vifuatavyo ni vyakula na vinywaji ambavyo vinatakiwa kuepukwa au kupunguzwa ili kujilinda na ugonjwa wa figo.

Vyakula vyenye mafuta mengi

Ulaji uliopitiliza wa mafuta mengi, hasa yale mabaya (saturated fats), huongeza mzigo na kuzorotesha afya ya figo.

Mafuta haya hupatikana zaidi kwenye bidhaa kama siagi na samli pamoja  na aina nyingine za mafuta ya mbegu yasiyo salama.

Mratibu wa Tiba na Magonjwa Yasiyoambukiza katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Dk Omari Mwangaza, anasisitiza umuhimu wa wananchi kuzingatia aina ya mafuta wanayotumia katika mapishi yao ya kila siku.

“Mafuta mazuri ni yale yenye omega-3, omega-6 au omega-9, ikiwa mafuta yako hayana hizo yana madhara,” anaeleza Dk Mwangaza.

Omega -3 ni mafuta ambayo yanapatika kwenye vyakula kama samaki wa bahari, 0mega-6 (alizeti) na omega-9 (mzaituni na  parachichi) yakisaidia kulinda afya ya moyo na kuboresha ustawi wa mwili kwa ujumla.

Vyakula vyenye chumvi (sodium) nyingi

Madini ya sodium yana jukumu la kudhibiti kiwango cha maji mwilini. Hata hivyo, yakizidi huweza kusababisha maji kubaki mwilini na kuleta madhara kama vile kuvimba kwa mwili, shinikizo la damu, uzito kuongezeka ghafla na matatizo ya kupumua.

Vyakula vyenye sodium nyingi ni pamoja na nyama iliyohifadhiwa kwa chumvi, samaki waliokaushwa kwa chumvi, soseji na ‘bacon’ ambazo wataalamu wa afya wanazitaja kuwa chanzo cha magonjwa ya figo.

Dk Mwangaza ameshauri  kudhibiti  vyakula vya chumvi kwa sababu milli ya watu wenye asili ya kiafrika huwa na mwitikio mkubwa zaidi katika matumizi ya chumvi na sukari 

Mtaalamu huyo wa afya amewarai Watanzania kujenga tabia ya kutoongeza chumvi mezani wakati wa kula chakula.

Unywaji wa maji/vinywaji venye sukari kupitiliza

Ingawa maji ni muhimu kwa mwili, kunywa kupita kiasi kunaweza kuwa na madhara hata kwa watu wenye figo zenye afya. 

Figo hufanya kazi ya kusafisha damu na kudhibiti maji na madini mwilini, na unywaji wa maji mengi huongeza mzigo na kupunguza ufanisi wa kawaida.

Tovuti ya Medical News Today inasema kuwa mbali na madhara ya moja kwa moja katika figo, unywaji wa maji mengi unaweza kushusha kiwango cha sodiamu kwenye damu (hyponatremia),kusababisha uchovu, maumivu ya kichwa,au matatizo ya fahamu kwa muda mfupi. 

Mbali na maji, Dk Mwangaza anaeleza kuwa unywaji wa vimiminika vingine vyenye sukari ikiwemo pombe zenye sukari kupitiliza huchochea uzalishaji wa sukari isiyohitajika kwenye mwili wa binadamu jambo linaloweza kumletea mtumiaji matatizo ya figo.

@jikopointtanzania

Sukari pombe ni aina ya sukari inayojulikana kisayansi kama Sugar alcohol au polyols. Ni kundi la vitu vya kemikali vinavyofanana na sukari lakini vina muundo unaofanana kidogo na pombe (alcohol) katika kemia. Jina ‘pombe’ hapa halimaanishi pombe ya kulewesha kama Ethanol. Ni neno la kemia tu kutokana na muundo wake. Mifano ya sukari pombe Baadhi ya aina zinazojulikana ni: Xylitol Sorbitol Maltitol Erythritol Zinatumika wapi? Sukari pombe hutumiwa sana katika: vyakula vya “sugar-free” au “no added sugar” pipi vinywaji vya diet baadhi ya dawa na dawa za meno SukariPombe SugarAlcohol Polyols Lishe Afya SugarFree Sweeteners Nutrition HealthyEating DiabetesCare#wafanyabiasharatanzania #soko #love #tende

♬ original sound – JikoPoint – JikoPoint

Vyakula vyenye protini nyingi

Protini inapovunjwa vunjwa mwilini hutengeneza mabaki kama vile urea, amonia na ‘creatinine’.

Kwa mtu mwenye matatizo ya figo, mabaki haya huweza kuongezeka na kuathiri zaidi utendaji wa figo.

Hivyo ni muhimu kupunguza ulaji wa protini nyingi na kuchagua protini zinazotumiwa kwa ufanisi zaidi na mwili, kama vile mayai, samaki, nyama, kuku, maziwa na jibini.

Vyakula vyenye protini ambazo huacha mabaki mengi ni pamoja na mbogamboga, matunda, maharage, kunde, mbaazi, mahindi, mtama, karanga, mkate.

/
No matches found for this filter
22 May, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
23 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
23 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

MIKOA YA KIPOLISI ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI TANZANIA BARA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

MIKOA 5 ILIYOONGOZA KWA MATUKIO BARABARANI 2025 TANZANIA BARA

Nukta TV