Sababu, Meta ikitangaza kuondoa ‘end-to-end encryption’ Instagram

March 17, 2026 2:56 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Huduma hiyo iitaondolewa kuanzia Mei 8, 2026
  • Yasema huduma ya jumbe za kificho itaendelea kuwepo kwenye mitandao yake mingine ikiwemo Whatsapp.

Dar es Salaam. Kampuni ya teknolojia ya Meta imethibitisha kuondoa huduma ya ujumbe wa kificho ‘end-to-end encryption’ kwenye mtandao wake wa kijamii Instagram ikibainisha mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa ujumbe wa mtandao huo.

‘End-to-end encryption’ ni mfumo wa usalama wa mawasiliano ambapo ujumbe au taarifa inafichwa kutoka kwa mtumaji hadi kwa mpokeaji pekee, na hakuna mtu mwingine anayeweza kuisoma katikati hata kampuni inayotoa huduma.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Machi 16, 2026 Meta imesema huduma ya ‘end-to-end encryption’ katika mtandao wa Instagram itafikia kikomo  Mei 8, 2026, ikiwataka watumiaji wake kupakua taarifa zao muhimu kabla ya wakati huo.

“Huduma ya ujumbe wa kificho ‘end-to-end’ kwenye mtandao wa Instagram itafikia mwisho Mei 8, 2026…iwapo una mazungumzo yanayoweza kuathiriwa na mabadiliko haya, utaona maelekezo ya jinsi unavyoweza kupakua picha, video au ujumbe wowote unaotaka kuhifadhi,” imeeleza taarifa ya Meta.

Meta pia imeeleza kuwa baadhi ya watumiaji watalazimika kusasisha (update) programu yao ya Instagram kabla ya kuweza kupakua mazungumzo yaliyokuwa yamefichwa.

Isabo Binde, mtaalamu wa masuala ya teknolojia jijini Dar es Salaam ameiambia Nukta Habari kuwa kuondolewa kwa ‘end-to-end encryption’ kutafanya jumbe na simu katika mtandao wa Instagram hazitakuwa tena faragha hivyo zinaweza kusomwa au kusikilizwa na mtu wa tatu (third party).

Sababu za kuondoa huduma

Taarifa za Meta zinaeleza kuwa huduma hii inasitishwa kwa sababu ya uhitaji mdogo baina ya watumiaji wa mtandao wa Instagram licha ya kuwa huduma inayotoa usalama na faragha.

Aidha, shinikizo la kisheria na kanuni duniani limekuwa likiongezeka kuhusu huduma za ujumbe zilizo na kificho, huku Serikali na wakaguzi wakionyesha wasiwasi kwamba huduma ya ‘end-to-end’ inaweza kuongeza ugumu wa kufuatilia shughuli haramu au kuzuia maudhui hatarishi.

Licha ya mabadiliko haya kwenye Instagram, Meta imesema huduma za kificho zitaendelea kuwepo kwenye mitandao mingine inayomilikiwa na kampuni hiyo, ikiwemo WhatsApp.

Kwa watumiaji wa Instagram wanaohitaji faragha kwenye jumbe na simu zao, majukwaa haya yanaweza kuwa mbadala salama mara huduma hiyo itakapofutwa mwishoni mwa mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV