Visima kumaliza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama nchini?

November 28, 2018 1:25 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Serikali imesema itachimba visima virefu na vifupi pamoja na kutumia maji ya maziwa na mita kuyapeleka katika maeneo mbalimbali ya wananchi nchini ili kumaliza hilo.
  • Wakuu wa wilaya zote nchini waagizwa kusimamia uhifadhi wa maeneo ambayo yana vyanzo vya maji ili kuyafanya yaendelee kuwa chepechepe, ili kuhakikisha vijiji vyote vinapata maji ya uhakika.
  • Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 inaelekeza kuwapatia wananchi waishio vijijini maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao

Dar es Salaam. Serikali imepanga kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa kuchimba visima virefu na vifupi pamoja na kutumia maji ya maziwa na mita kuyapeleka katika maeneo mbalimbali ya wananchi nchini.

Mpango huo umetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo (Novemba 27, 2018) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule sekondari Bugando kata ya Nzera wilayani Geita, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi za siku nne mkoani Geita.

Amewaagiza wakuu wa wilaya zote nchini kusimamia uhifadhi wa maeneo ambayo yana vyanzo vya maji ili kuyafanya yaendelee kuwa chepechepe, ili kuhakikisha vijiji vyote vinapata maji ya uhakika.

Kwa mujibu wa wizara ya Maji na Umwagiliaji, hadi sasa miundombinu ya maji iliyojengwa ina vituo vya
kuchotea maji 123,888 ambavyo vina uwezo wa kuhudumia watu milioni 30.9 sawa na asilimia 85.2 ya wananchi milioni 36.34 waishio vijijini. 

Hata hivyo, vituo 85,286 tu ndivyo vinavyofanya kazi na kutoa huduma kwa watu milioni 21.32 sawa na asilimia 58.7 ya wananchi waishio vijijni.

Serikali kupitia Kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.


Zinazohusiana: Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano utunzaji bonde la mto Nile


Amesema Serikali imejipanga vizuri kuhakikisha kila kijiji kinapata huduma ya maji safi na salama, hivyo amewaagizawatendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yote yenye misitu na vyanzo vya maji na kuhakikisha yanalindwa.

Naye, Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini, Joseph Musukuma ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miradi ya maji, umeme na hospitali  katika jimbo lake.

“Nashukuru Serikali pia kwa kutuzindulia hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Geita,” amesema Msukuma.

Maji ni uhai, mtu akiyakosa maisha yake yanakuwa mashakani.

Sera ya Taifa ya Maji ya mwaka 2002 inaelekeza kuwapatia wananchi waishio vijijini maji safi na salama katika umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao. Lengo ni kufikia asilimia 85 ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi na salama katika maeneo ya vijijini ifikapo mwaka 2020.

“Hali hiyo imechangiwa na changamoto ya mfumo uliopo wa usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji'” alinukuliwa aliyewahi kuwa waziri wa Maji, Mhandisi Isack Kamwele wakati akisoma hotuba ya bajeti ya mwaka 2018/2019 bungeni Jijini Dodoma.

Enable Notifications OK No thanks