Vijana, wanahabari changamkieni masomo ya takwimu -Nuzulack Dausen

February 2, 2019 4:24 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link

Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa, Nuzulack Dausen (katikati) akiwa kwenye mahojiano kuhusu matumizi ya takwimu katika maisha ya kila siku na maendeleo ya taifa katika studio za Kiss FM Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Takwimu husaidia katika kutekeleza mipango mbalimbali katika ngazi ya mtu, kaya hadi taifa. Picha| Zahara Tunda.


  • Awashauri wamahabari wajifunze jinsi ya kuripoti habari za takwimu ili kuwa na thamani katika soko la ajira.
  • Awataka kufuata sheria za takwimu na kutumia vyanzo vya takwimu vinavyojulikana na kutambuliwa na serikali ili kuepuka kujiingiza kwenye matatizo yasiyo na msingi.

Dar es Salaam. Kutokana umuhimu wa matumizi ya takwimu katika kufanya maamuzi sahihi, Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa Nuzulack Dausen amewaasa vijana wanaoenda kujiunga na vyuo vikuu kusoma masomo yanayohusu takwimu na teknolojia ili waweze kuendana na soko la ajira huku akitoa rai kwa waandishi wa habari kubobea katika sekta hiyo.

Dausen amezungumza hayo kupitia mahojiano ya kipindi cha  Morning Kiss cha  Radio Kiss FM, Dar es Salaam juu ya umuhimu wa matumizi ya takwimu kwa wananchi na waandishi wa habari hapa nchini.

Mkurugenzi huyo amesema matumizi ya takwimu kwa zama hizi ni makubwa kutokana na kukua kwa teknolojia na mahitaji ya watu kupata taarifa ili kusaidia katika mipango mipango mbalimbali ya kimaendeleo.

Mbali na umuhimu huo katika kufanya maamuzi, amesema kuwa kasi ya kuongezeka kwa habari za usushi (fake news) inafanya wanahabari wajao na walaji wa habari kuwa na ufahamu mkubwa wa matumizi ya takwimu ili kukabiliana na uzushi huo.

“Takwimu zinatupa ufahamu wa hali halisi ya vitu vinavyoendelea katika jamii na kwa kiasi gani tunaweza kufanya maamuzi sahihi na kujua ukweli kwa ajili maendeleo yetu,” amesema Dausen.

Takwimu ni moja ya nyenzo muhimu ambayo husaidia watu, taasisi na Serikali kufanya maamuzi katika nyanja mbalimbali za maisha na sasa nchi nyingi na mashirika makubwa yanawekeza kiwango kikubwa cha fedha ili kuzalisha takwimu bora na zinazopatikana kirahisi hasa kupitia mifumo ya dijitali.

Kuhusu umuhimu wa takwimu katika sekta mbalimbali kama ya elimu, Dausen alitolea mfano namna uchambuzi wa matokeo ya mitihani na upangaji wa shule ya kwanza hadi ya mwisho unavyosaidia wadau wa elimu kama wazazi kufanya maamuzi sahihi pale wanapotaka kupeleka watoto wao kwenye shule za msingi au sekondari.

Ukiondoa sekta ya elimu, amesema matumizi ya takwimu pia ni muhimu katika kilimo ambapo zinasaidia wakulima kujua mwenendo wa soko la mazao yao ndani na nje ya nchi na uhitaji wa bidhaa sokoni kwa kupitia uchambuzi na tafiti mbalimbali ambazo huzalisha takwimu mahususi.


Zinazohusiana: Wanahabari wahimizwa kuripoti habari za nishati jadidifu

                         Weledi, takwimu sekta ya nishati kuwatoa Wanahabari Tanzania


Hata hivyo, amewataka wataalam hasa wale wanaotoa taarifa mbalimbali kama wanahabari  kujihusisha moja kwa moja kwenye kubobea kuandika habari za takwimu au kuzichambua kwa kina ili kuwaletea suluhisho watu wa hali ya chini kwenye kuamua mambo yenye maslahi kiuchumi.

”Kwa vijana hasa wale wanaosoma mambo ya habari natoa rai waweze kujifunza masuala ya takwimu ili  kujiongezea nafasi ya kupata ajira katika soko la ushindani kwa kuwa ‘data is a new oil (takwimu ni yana thamani kubwa kama ilivyo mafuta,” amesema Dausen.

Pamoja na hayo amewashauri wanahabari kutokuwa waoga katika kuandika habari za takwimu bali wafuate sheria na watumie vyanzo vya kuaminika vinavyotambuliwa na Serikali kwenye kupata taarifa zao.

“Kama mwanahabari au mdau wa takwimu inabidi ujiridhishe kuhusu takwimu hizo unazotaka kuzitumia…lazima ufanye utafiti wa kina na kujiridhisha chanzo chake…kumbuka sheria ya takwimu bado ipo na ni lazima kuifuata,” amesema Dausen ambaye ameshinda tuzo mbalimbali za uandishi wa habari ndani na nje ya nchi ikiwemo ya mwandishi bora wa habari za takwimu mwaka 2017 nchini kwa upande wa magazeti.

Nukta Africa ni kampuni ya habari na teknolojia iliyojikita katika uzalishaji wa habari za mtandaoni, kutoa mafunzo ya uwasilishaji takwimu, utengenezaji wa mifumo ya dijitali na ushauri elekezi katika masuala ya habari. Kampuni hiyo humiliki pia tovuti ya habari ya Nukta (nukta.co.tz) inayoangazia habari na makala za kiuchambuzi kuhusu uchumi, biashara, teknolojia, utalii, takwimu na maendeleo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV