Uvaaji wa barakoa muda mrefu hausababishi uhaba wa oksijeni mwilini

June 12, 2020 8:18 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakikisha umevaa vizuri barakoa yako kiasi cha kusitiri pua na mdomo.
  • WHO imesema uvaaji wa muda unaweza kuwakera wengi ila hauna madhara kama inavyodaiwa.

Dar es Salaam. Miongoni mwa habari unazotakiwa kuzipuuzia kipindi hiki ni pamoja na ile inayosema uvaaji wa barakoa kwa muda mrefu unasababisha ukosefu wa hewa ya oksjeni mwilini na kuongeza sumu kutokana na kuvuta hewa chafu ya dioksidi kaboni (carbon dioxide).

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeeleza kuwa habari hiyo haina ukweli wowote uliothibitishwa kisayansi.

“Uvaaji wa muda mrefu wa barakoa kuna wakati unakera lakini hausababishi madhara kwa kuvuta hewa ya dioksidi kaboni au kusababisha ukosefu wa oksijeni mwilini,” imesema WHO.

Shirika hilo linaeleza kuwa yakupasa uvae vema barakoa yako kwa kuhakikisha unasitiri pua na mdomo wako vizuri kiasi cha kukuwezesha kupumua vema.

“Usitumie zaidi ya mara mbili barakoa inayopaswa kutumika kwa muda mfupi na kutupwa (disposable masks) na jitahidi kuibadilisha mara utakapoona imeshika uchafu au kuwa umefika maeneo hatarishi yenye corona,” limesema shirika hilo ambalo hutoa miongozi ya kiafya ulimwenguni.  

Tufuate kwenye mitandao yetu Twitter, Facebook @NuktaFakti na Instagram @nuktafakti kwa taarifa zaidi kuhusu habari sahihi za corona. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV