Utambuzi wa ng’ombe unavyofanyika Tanzania

November 15, 2021 11:16 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  •  Ni kwa kuwapiga chapa, rangi na kuwavalisha heleni.
  • Njia hizi husaidia kuwalinda wanyama hao dhidi ya wezi.
  • Pia ni njia rahisi ya kujua idadi ya ng’ombe wanaomilikiwa. 

Dar es Salaam. Utambuzi na ufuatiliaji wa wanyama imekuwa ni njia rahisi ya kutunza kumbukumbu za mifugo kupitia usajili wa mifugo yenyewe, wamiliki wake, mahali ilipo na matukio muhimu kwenye uhai wa mifugo hiyo.

Nchini Tanzania njia tano hutumika katika utambuzi wa wanyama wa kufugwa wakiwemo ng’ombe ni kupiga chapa, ukoo wa ng’ombe, rangi, heleni za masikioni na ukataji sehemu ya masikio.

Njia hizo zimekuwa zikitumiwa na wafugaji katika maeneo mbalimbali Tanzania ambapo utambuzi wa ng’ombe unaweza kuwa wa mnyama mmoja mmoja au wa kundi kwa maana ya alama moja kwa kundi la wanyama.

Pia utambuzi wa wanyama kwa kundi unafanyika kwa kila kijiji kuwa na alama moja ya chapa ya utambulisho wa kitaifa. Njia hizo pia hutumika kudhibiti wizi wa mifugo.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Sensa ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2019/20, jumla ya ng’ombe milioni 1.9 wanaofugwa katika kaya za Tanzania walilipotiwa kutambuliwa kwa njia mbalimbali ikiwemo upigaji chapa.

Ng’ombe 55,925 kati ya hao walitambuliwa visiwani Zanzibar. Ni njia gani inayotumika zaidi katika utambuzi wa ng’ombe nchini Tanzania?

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV