Unavyoweza kuboresha kasi simu ya mkononi

December 13, 2024 5:01 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa kufanya maboresho kasi ya michoro kupitia mpangilio wa simu yako 

Dar es Salaam. Je, umechoshwa na kasi ndogo ya utendaji kazi wa simu yako wakati unaperuzi, unahama kutoka ‘App’ moja kwenda nyingine au unapotazama picha na video? 

Kwa mujibu wa tovuti ya ZDNET inayotoa habari, uchambuzi na maelezo ya teknolojia na bidhaa zake, kuna mbinu rahisi ya kukuwezesha kuifanya simu hiyo kuwa na kasi mara mbili zaidi kwa kila aina ya simu za Android.

Ni kupitia marekebisho ya kasi ya michoro (animation speed), mbinu hii ni ya haraka, bure na inayofungua wigo mpana wa kufanya mambo yako kwa haraka na kuokoa muda.

Ni rahisi

Kinachohitajika ni simu ya Android, nenosiri, PIN, au mchoro wa skrini yako ya kufungua simu (pattern) ili kufungua kipengele kinachoitwa  ‘developer options’ ambapo hapo ndio utaweza kuongeza au kupunguza kasi ya simu yako.

Fungua developer options

Ili kufikia animation speed, unahitaji kufungua kwanza ‘developer options’, menyu ambayo kikawaida imefichwa, ikiwa ni mahususi kwa watengenezaji wa programu lakini iko wazi kwa yeyote anayependa kuitumia.

Ili kufika kwenye kipengele hicho fungua mipangilio ya simu (Settings) kwenye simu yako kisha shuka chini na gusa kuhusu simu au neno (about phone) kisha tafuta ‘software information’ na uguse sehemu iliyoandikwa build number ambapo utaibonyeza mara saba. 

Mwonekano wa mpangilio ukionesha vipengele vinavyotumika kuongeza kasi ya simu. Picha| Kerry Wan/ZDNET

Ikiwa ni mara yako ya kwanza, ujumbe utaonesha idadi ya ulizobonyeza na  ukimaliza, utaona ujumbe ukithibitisha kwamba developer options zimewezeshwa.

Ili kukipata tena kipengele hichi utapaswa kurudi kwenye ukurasa wa mwanzo wa mipangilio ya simu  ‘Settings’ kisha shuka chini kabisa na kufuata hatua kama zilivyoelekezwa huko juu.

Rekebisha kasi 

Baada kuwezesha kipengele cha ‘developer options’ ni wakati sasa wa kufanya simu yako iwe nyepesi kwa kufuungua ‘developer options’ ndani ya setting ya simu shuka mpaka kwenye sehemu ya ‘drawing kisha tafuta three drawing setting.

Hapo utaona setting hizo ambazo ni Window animation scale hii nadhibiti kasi ya programu na jumbe  nyingine ni transition animation scale hii inadhibiti kasi ya mabadiliko kati ya skrini au programu pamoja na animator duration scale ambayo huathiri michoro ya jumla ya UI, kama kufungua na kufunga programu au kutoa nenosiri kwenye simu yako.

Unachotakiwa kufanya ni kugusa kila kipengele na ubadilishe namba kutoka 1x hadi 0.5x ambapo kadri namba inavyokuwa ndogo, ndivyo kasi inavyoongezeka.

Baada ya kufanya mabadiliko hayo jaribu kuperuzi simu yako, fungua programu, na fanya shughuli zako za kawaida unapaswa kuona tofauti ya papo hapo katika mwitikio wa simu na ikiwa bado unaweza kumuona mtaalamu wa vifaa vya kielekitroniki.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Nukta TV

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV