Njia salama za matumizi ya simu ya mkononi

August 14, 2021 7:23 am · Anoth
Share
Tweet
Copy Link
  • Hakikisha simu yako haithiri afya na maisha yako.
  • Zingatia matumizi sahihi ya simu ikiwemo kupunguza mazungumzo marefu.

Dar es Salaam. Simu janja na simu zingine za kawaida ni vitu ambavyo haviepukiki  katika maisha  yetu ya kila siku. Kifaa hicho cha mawasiliano kimesaidia kufanikisha mambo mengi ikiwemo kuimarisha mahusiano ya watu.

Licha ya mazuri yote yanayofanywa na simu ya mkononi lakini bado ina madhara makubwa kwa afya ya mwanadamu hasa kama matumizi sahihi na salama hayajazingatiwa.

Zifuatazo ni njia salama za kutumia simu yako ya mkononi ili kuepuka madhara mbalimbali yakiwemo ya kiafya:

Zuia mazungumzo ya muda mrefu

Sote tutakubaliana kwamba ukitumia mazungumzo yako ya muda mrefu kupitia simu ni dhahiri simu huchemka na kuzalisha mionzi ambayo hupenyeza kwenye seli za damu na kwenda kuharibu tishu kwenye ubongo, ngozi na hata masikio.

Madhara haya yanaweza kuwa kuumwa kichwa, uchovu na baadaye kupata hata saratani. Hakikisha unafanya mawasiliano ya simu pale inapohitajika. 

Pia watoto wadogo wasimamiwe katika matumizi ya simu ili wasiongee muda mrefu ili kuwaepusha na madhara ya kiafya ikiwemo kuathirika kwa ubongo.

Simu isipotumiwa vizuri inaweza kuwa sehemu ya kuleta madhara kwa afya yako. Picha| Nukta Africa.

Tumia spika za masikioni wakati wa kuwasiliana

Matumizi ya spika za masikioni zisizo na waya (wireless headphones) pia matumizi ya ‘bluetooth’ ni njia nzuri zaidi ya kutumia kwasababu hazizalishi mionzi hatarishi kwenye afya yako. 

Unaweza pia kufanya mazungumzo bila kuiweka simu yako masikioni na ukatumia sauti ya juu (loud speaker) ili kupunguza mashara kwenye sikio lako.

Weka mbali simu na mwili wako

Mara nyingi mtu akimaliza kutumia simu analala nayo kitandani, hii ni hatari kwa afya yako, na hii siyo simu tu ni vifaa vyote vinavyopitisha umeme ni lazima vikae mbali na mwili wa binadamu.

Unapolala na simu fahamu kuwa mitandao ya simu bado inatuma mawimbi  kwenye simu ili kuhakikisha simu yako inakuwa hewani. Hii ndiyo chanzo cha mionzi inayoweza kuzalishwa na baadaye kukuathiri kama utakuwa na kifaa hiki kwenye mwili wako.

Zima data baada ya matumizi

Inashauriwa baada ya kutumia simu yako na unataka kulala zime miunganiko ya aina yoyote kwenye simu yako kama vile Bluetooth na vifaa vinavyokuwezesha kupata inteneti kwenye simy yako ikiwemo ‘router’ na Wi-Fi. 

Hii itasaidia kupunguza mionzi isikufikie kirahisi na pia kupunguza gharama za intaneti.

Ukilala weka mbali simu yako kuepusha mionzi kukufikia kirahisi. Picha| inf.news.

Usiongee na simu sehemu zenye mtandao hafifu

Sehemu zenye mtandao hafifu hapa ndipo simu hulazimika kutoa mionzi mingi isiyo ya kawaida ili kuunganisha na mtandao wa simu  kitu ambacho ni hatari kwa mtumiaji wa simu anayeongea.

Tumia njia ya ujumbe zaidi kuliko kuongea

Inashauriwa kutumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) ni njia salama zaidi ya kutumia simu kwani hapa mwili huwa mbali na simu lakini pia mionzi inayotoka huwa ni kidogo au hafifu, pendelea kutumia barua pepe au hata ujumbe wa kawaida.

Tumia chanja inayoendana na simu yako

Kuzuia shoti za umeme na hata simu yako kuharibika mapema, tumia chaja inayopendekezwa na watengenezaji wa simu. Unapotumia chaja isiyoendana na simu yako unajiweka katika hatari ya kupoteza simu yako na hata msuaguano wa umeme. 

Hata hivyo, kila mtu ana matumizi yake ya simu, lakini tunatakiwa tuwe na kiasi ili tuwe salama wakati wote.

Enable Notifications OK No thanks