Uzingatie nini unapotengeneza kashata za tambi?

July 19, 2024 1:15 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Kashata za tambi hujulikana kama vileja vya tambi.
  • Hakikisha una mahitaji yote muhimu ikiwemo tambi na zabibu. 
  • Ni chakula maarufu katika mikusanyiko ya watu.

Vileja vya tambi. Ndio! Ni aina ya chakula kinachopendwa na watu wengi kwa sababu kina aina mbalimbali ya mapishi.

Kuna vileja vya aina mbalimbali vikiwemo vya nazi, ngano na hata tambi. 

Leo nitakufundisha kwa undani unavyoweza kupika vileja vya tambi na mambo ya kuzingatia ili kupata matokeo mazuri katika pishi lako. 

Vileja hujulikana kama kashata lakini zinategemea umetumia bidhaa gani ya chakula kutengeneza.

Tuingie jikoni

Hatua ya kwanza ni wewe kuweka karai kwenye moto kiasi kisha weka siagi yako. Baada ya hapo weka tambi uzikaange na uziachie mpaka ziwe rangi ya dhahabu unaweza kutumia dakika 5 mpaka dakika 7.

Ongeza rozi na zabibu huku unakoroga kisha weka maziwa ukiendelea kukoroga. Ongeza arki ili kuongeza ladha. 

Hatua inayofuata ni kuepua karai, tumia kijiko kuchotea na weka kashata zako kwenye  kikombe cha kahawa nusu usikijaze kisha kipindue kwenye sahani utoe kileja.

Rudia hatua hiyo mpaka umalize vyote na ukimaliza  vileja vitakuwa tayari kwa kuliwa.

Unasubiri nini? Leo andaa vileja vya tambi ili kuwafurahisha wapendwa wako nyumbani. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV