Namna ya kupika ‘zege’ la tambi za mayai

May 31, 2023 10:39 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Pishi hili linaweza kuwa mbadala wa chipsi mayai
  • Ni rahisi kuandaa na mahitaji yake ni machache

Zege la tambi za mayai ni moja kati ya aina mpya ya chakula inayojizolea umaarufu kwa kwa baadhi ya wapishi wasiopenda kukaa muda mwingi jikoni.

Ikiwa utakula chakula hiki kwa mara ya kwanza pasi na shaka unaweza kudhani ni chipsi mayai au ‘zege’ kama wengi wanavyopenda kuliita.

Kuanzia maandalizi,muda wa kuandaa na muonekano wake kwa ujumla  pishi hili linafanana sana na pishi la  chipsi mayai.

Kwa wauzaji wa hoteli,migahawa na ‘mama ntilie’ wanaweza kuongeza pishi hili linaloweza kuwaongezea wateja wanaokipenda chakula hicho.

Tusogee jikoni tujifunze mbinu rahisi za kuandaa ‘zege’ la tambi mayai.

Maandalizi

Mapishi yetu ya tambi za mayai yanaanza kwa kuandaa kuchemsha maji kiasi kwa ajili ya kuchemshia tambi kabla ya kuzikaanga na mayai.

Maji yakichemka weka tambi na uziache jikoni kwa dakika 3 mpaka 5 kutokana na wingi wa tambi zako. Baada ya hapo zichuze na uziache wazi zipoe.

Hatua inayofuata ni kuandaa mayai kwa kuyapasua na kuyakoroga mpaka yachanganyike vizuri, kisha menya nyanya,kitunguu na hoho utakavyo vitumia katika pishi lako.

Baada ya kumaliza maandalizi hayo changanya tambi ulizozichemsha, chumvi kiasi na viungo vyote ulivyoviandaa. Hakikisha vimechanganyika vizuri kabla ya kuweka jikoni.

Bandika kikaango weka mafuta kiasi ikifuatiwa na tambi pamoja na viungo ulivyochanganya, mimina mayai kwa juu (kama unavyomimina wakati wa kukaanga chipsi mayai) kisha acha yaive.

Baada ya dakika tatu geuza tambi taratibu kwa kijiko kipana ili zege lako lisivurugike kisha acha upande huo uive kwa dakika mbili nyingine.

Ili zegelako liive vizuri tumia kijiko kusukuma kwa juu ili kuruhusu  sehemu ya ndani ya tambi na mayai kuiva.Hatua hii pia itasaidia tambi kukauka vizuri.

Mpaka hapo pishi lako lipo tayari kwa kula unaweza ukasindikiza na soda, juisi au chai.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Nukta TV

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Nukta TV