Umekuwa ukijibebea vitu hotelini? Hivi ndivyo vitu unavyoruhusiwa

February 12, 2020 7:56 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Sabuni za kuogea, losheni na dodoki. Hivyo ni vyakwako, beba!
  • Umewahi “kusepa” na taulo la hotelini? Aibu yako.
  • Kama kuna kitu umekipeda, uliza kama unaweza kukichukua.

Dar es Salaam. Kama wewe ni mtu wa kusafiri ambaye mara kwa mara unafikia  hotelini, huenda umekutana na vitu vyenye kukujaribu na kuifanya mikono yako igandamane navyo.

Lakini usicho kijua ni kwamba, wakati ukiendelea kujihisi mdokozi, vipo vitu ambavyo vimewekwa kwaajili ya matumizi yako na hakuna ambaye ataweza kuvitumia tena  baada ya wewe kuviacha hata kama vimebaki.

Kwanini uache vitu hivyo  vitupwe wakati begi lako lina nafasi ya kuvichukua? Kama wewe umekuwa ukichukua vitu hivi, basi wala sio mdokozi bali umekuwa ukijiibia mwenyewe.

Sabuni za kuogea na miswaki

Haijalishi ni sabuni ya aina gani ama  iliyopo kwenye mfumo wa mche au la utakayoikuta hotelini hiyo imewekwa kwaajili yako tu na hakuna mgeni atakaye ingia na kuitumia. Itatupwa.

Kama hoteli uliyofikia imekuwekea sabuni, dawa ya meno na hata mswaki, hivyo ni vyako. Beba!

Dodoki na “toilet paper”

Unahisi kuna mtu atakaye kuja kuogea dodoki lako? Hoteli huwa na kawaida ya kuweka dodoki jipya kwaajili ya kila mgeni anayekuja. Kama umebahatika kuingia hoteli yenye mapenzi na wewe kiasi cha kukuwekea dodoki hilo ni lako. Pokea zawadi hiyo inayokuja bila kifungashio.

Toilet paper nayo hiyo ni yako. Beba itakusaidia kwenye safari yako na hata nyumbani kwako.

Maji ya kunywa na steshenari

Kwenye meza yako, huenda umekuta maji ya kunywa na kijidaftari na kalamu yake. Mara nyingi hoteli hukuwekea vitu hivi kwani wageni wengi huvisahau.

Kama hujagundua, vijidaftari hivi huwa na nembo ya hoteli hivyo ni mojawapo ya njia ambazo hoteli huzitumia kujitangaza.

sabuni ya aina gani ama  iliyopo kwenye mfumo wa mche au la utakayoikuta hotelini hiyo imewekwa kwaajili yako tu na hakuna mgeni atakaye ingia na kuitumia. Itatupwa. Picha| Twitter.

Losheni, vitana na ndala

Hapana! Siongelei kandambili. Naongelea zile ndala ambazo zinatumika mara moja tu. hizo ni zako zichukue kwani ukiziacha zitatupwa. Losheni ndogo ambayo hoteli imekuwekea, ni zawadi yako. Mara nyingi unapoziacha, huenda unawazawadia “house keeping” bila kufahamu. Pokea zawadi hiyo itakusaidia njiani nasa kama unavijisafari vinavyoendelea.

Huna haja ya kuingia gharama za kununua mafuta baada ya kuacha zawadi uliyopewa.

Kama kuna kitu ambacho kimekuvutia hauna haja ya kujikuta jambazi mdogo. Muulize mhudumu wa hoteli hiyo kama unaweza kuchukua. 

Baadhi ya hoteli huweka vitu kama miamvuli, na hata vijibegi kwaajili yako lakini wengi huogopa kuchukua kwa kuhofia kuwa wataitwa wezi.kama hauna uhakika wa kitu hicho kuwa mali yako, uliza tu, hautokufa.

Umeona vitu vilivyowekwa kwaajili yako. Ni wasaa wa wewe kuvijua vitu ambavyo unatakiwa kutumia na kuviacha.

Naongelea zile ndala ambazo zinatumika mara moja tu. hizo ni zako zichukue kwani ukiziacha zitatupwa. Picha| Pinterest.

Taulo na mashuka

Umekuta taulo hotelini na limekuvutia na ukajifanya kufumba macho wakati unalipakia kwenye begi. Aibu yako! Kwa mataulo mengi yanayowekwa hotelini, yawe ya kukaushia uso na hata mwili, yamewekwa kwa matumizi ya kuendelea. Ukiondoka, taulo na shuka litafuliwa kwaajili ya mtu mwingine.

Vifaa vya kutundikia nguo (hanger)

Kwenye kabati la hotelini, hoteli imekujali na kukuwekea vifaa vya kutundikia nguo zako ili zisijikunje. Vifaa hivyo vimewekwa kwaajili ya matumizi yako na pia ya mgeni anayekuja. Viache!


Zinazohusiana


Mapambo ya hotelini

Huenda umewahi tembelea moja ya hoteli na kukuta vijimapambo kitandani na mezani kwako.

Hoteli imekuwekea vitu hivyo kukukaribisha tu na siyo kwaajili ya wewe kuvichukua.

Huenda una getto au nyumba ambayo itapendeza na mapambo hayo lakini jaribu kununua mapambo yako. Kama umevutiwa sana na picha za ukutani, ulizia mhudumu wapi unaweza kuzipata kama hizo ili na wewe ukapambe nyumba au getto lako.

Vikombe na glasi

Hoteli nyingi huweka vikomba hasa kama nchi au eneo hilo lina hali ya ubaridi. Pamoja na vitu hivyo, hoteli huweka vijifuko vya majani ya chai na sukari au kahawa kwaajili yako. Chukua chai zako na sukari zako lakini tafadhali acha kikombe na glasi chumbani.

Japo zipo hoteli zinazoweza kukuzawadia kikombe lakini ni vyema ukauliza kwani baadhi ya hoteli hufanya hivyo  kwa ajili ya matangazo. Uliza kama ni chako utapewa.

Baada ya kuisoma makala hii huenda ukaacha kujiita mwizi kwa zile losheni ambazo umekuwa ukibeba ukienda hotelini na kwa wewe ambaye ulisepa na kikombe cha watu, aibu yako. 

Zidi kusoma Nukta habari kwa mambo yanayokuhusu.

Enable Notifications OK No thanks