BoT yatangaza nafasi za ajira 83

March 12, 2026 6:21 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Waombaji watakiwa kutuma maombi yao kupitia mfumo rasmi wa maombi ya ajira wa Serikali.

Arusha. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza nafasi za ajira 83 katika fani mbalimbali kwa Watanzania wenye sifa, ujuzi na uwezo wa kuchangia katika utekelezaji wa majukumu ya benki hiyo.

Taarifa ya Dk Rahma Mahfoudh, Naibu Gavana Utawala na Udhibiti wa Ndani wa BoT iliyotolewa leo Machi 12,2026 imebainisha kuwa nafasi hizo zimeandaliwa ili kuimarisha utoaji wa huduma, kuongeza ufanisi wa kiutendaji na kuendeleza nguvu kazi yenye weledi, ubunifu na maadili ya utumishi wa umma.

Nafasi hizo zilizotangazwa na BoT zimewekwa katika mfumo rasmi wa maombi ya ajira wa Serikali zikihusisha nafasi mbili za mhudumu wa jikoni daraja la tatu, mlinzi III (13), afisa sheria III (2), mratibu wa programu/mkufunzi III (1), mpagazi III (2), mchambuzi wa mifumo ya kompyuta/programu III (5) na nafasi nne za mkaguzi wa ndani wa mifumo daraja la tatu.

Nafasi nyiingine ni afisa usalama III (2), afisa mipango III (1), na mchambuzi wa masuala ya fedha III (1), katibu Muhtasi III (3), fundi usanifu TEHAMA III (6), mhandisi mitambo III (1), mhandisi umeme III (1), mhudumu wa mapokezi III (4), afisa ugavi na ununuzi III (2), afisa rasilimali watu III (3) na nafasi nane za wahasibu III.

Aidha, tangazo hilo limehusisha nafasi 13 za afisa benki daraja la tatu mkaguzi wa benki III (6) fundi sanifu umeme III (1), fundi sanifu elektroniki III (1) na nafasi moja ya mchambuzi wa biashara la tatu.

BoT imewahimiza waombaji  kuwasilisha maombi yao kupitia tovuti ya https://portal.ajira.go.tz/vacancies kabla ya Machi 24, 2026 huku sifa za waombaji zikianishwa katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV