Ufaulu matokeo ya darasa la saba waongezeka kiduchu

November 23, 2023 10:30 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Waongezeka kwa asilimia 0.96.
  • Idadi ya wavulana na wasichana waliofaulu yaoana.
  • Wenye mahitaji maalum waongezeka.

Dar es Salaam.Baraza la MitihaniTanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani ya darasa la saba kwa mwaka 2023 huku ufaulu wa jumla ukiongezeka kidogo kwa asilimia 0.96 kulinganisha na mwaka 2022.

Katibu mtendaji wa Necta, Dk. Said Mohamed aliyekuwa akitangaza matokeo hayo leo Novemba 23, 2023 jijini Dar es Salaam amesema ufaulu wa jumla umeongezeka kutoka asilimia 79.6 waliofaulu mwaka jana hadi 80.5 mwaka huu.

“Ufaulu wa jumla umepanda kwa asilimia 0.96 na nakufikia asilimia 80.5 ya watahiniwa wote  ambapo watahiniwa 1,092,960  wote wamefaulu kwa kupata madaraja ya A, B na C,” amesema Dkt Msonde.


Soma zaidi:Necta yatangaza matokeo ya darasa la saba 2023.


Watahiniwa milioni 1.3 wa darasa la saba walisajiliwa kufanya mtihani wa Taifa uliofanyika Septemba 13 na 14 mwaka huu ambapo wavulana walikuwa 654,603 sawa na asilimia 46.8.

Kwa mujibu wa Dk.Mohamed idadi ya wavulana na wasichana waliofaulu haitofautiana sana ukilinganisha na miaka ya nyuma ambayo wavulana waliofaulu walikuwa wengi kushinda wasichana.

“Kuhusu ulinganifu wa ufaulu kijinsia takwimu ziaonyesha kuwa hakuna tofauti kubwa ya ufaulu kati ya watahiniwa wavulana na wasichana kwani wote wamepata ufaulu unaokaribiana wa 80.58 kwa Wasichana na kwa 80.59 wavulana,” ameongeza Dkt Mohamed.

Aidha, watahiniwa wenye ulemavu walikuwa walikuwa 4,599 sawa na asilimia 0.33 ya watahiniwa wote waliofanya mitihani. Idadi hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 8.9 kutoka idadi wa wenye ulemavu waliofanya mtihani mwaka jana.

Akizungumzia ongezeko hilo la wenye mahitaji maalum  Dk. Mohamed amesema jitihada mbalimbali zinaoendelea kuhakikisha wanatambua mahitaji yao ya mtihani yanatekelezwa ipasavyo.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV