Necta yatangaza matokeo ya darasa la saba 2023.

November 23, 2023 7:44 am · admin
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2023 ambapo jumla ya watahiniwa milioni 1.3 wamefaulu kwa kupata madaraja a, b, na c.

Katibu Mtendaji wa NECTA Dk. Said Mohamed aliyekuwa akitangaza matokeo hayo leo Novemba 23, 2023 amewaambia wanahabari kuwa asilimia 76 ya waliofaulu wamepata daraja b na c.

“Ufaulu umeongezeka kidogo kwa asilimia 0.96 na kufikia asilimia 80.6,” amesema Dk. Mohamed

Bofya hapa kutizama matokeo ya darasa la saba 2023


Enable Notifications OK No thanks