Ufanye nini ukikutana na habari za uzushi mtandaoni

September 17, 2025 2:48 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kuripoti kwa mamlaka husika au kuwasiliana na wathibitisha habari.

Arusha. Taarifa za uzushi zimetapakaa kila mahali hususani katika mitandao ya kijamii ambayo watumiaji wake wanazidi kuongezeka nchini Tanzania.

Ukiwa miongoni mwa watumiaji wa mitando hiyo zipo hatua hadhaa za kuchukua unapokutana na taarifa za uzushi kutoka katika chanzo chochote kupitia mitando ya kijamii.

Hatua hizo ni pamoja na  kutokuisambaza kwa watu wengine, kwa kufanya hivyo utakua umeokoa maisha ya ndugu, jamaa na marafiki.

Unaweza pia kuripoti taarifa hiyo kwa kwa mamlaka husika ili kukusaidia kuthibitisha na kuweka wazi ukweli wa habari husika ya uchaguzi au ukawasiliana na wathibitisha habari walio karibu yako.

Hata baada ya kufanya hayo usisahau kuithibitisha taarifa hiyo mwenyewe kwa kuangalia vyanzo vingine vya habari ili kujiridhisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow Us on TikTok

Subscribe to Our YouTube Channel

Subscribe

Loading videos...

Loading videos...

Loading videos...

Enable Notifications OK No thanks