Uchumi wa Tanzania kukua kwa asilimia 5.5 mwaka 2020

June 11, 2020 6:03 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Matarajio hayo yapo juu kidogo kutoka ukuaji wa asilimia 4 uliokuwa ukitarajia awali kutokana na madhara ya corona.
  • Ikumbukwe kuwa uchumi mwaka 2019 ulikuwa kwa wastani wa asilimia 7.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha Dk Philip Mpango amesema kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania inatarajiwa kupungua kidogo hadi  asilimia 5.5 mwaka 2020 kutoka kwenye maoteo ya awali ya asilimia 6.9.

“Kwa mwaka 2020 ukuaji wa pato la Taifa unatarajiwa kupungua kidogo kutoka kwenye maoteo ya awali ya asilimia 6.9 hadi asilimia 5.5 kutokana na hatua madhubuti zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais John Magufuli na hususan kuhimiza wananchi waendelee kufanya kazi wakati wanaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya corona kama ilivyoelekezwa na wataalamu wa wa afya pamoja na matarajio ya kuimarika kwa uchumi wa kikanda na dunia,” Dk Mpango ameliambia Bunge Alhamis, Juni 11, 2020. 

Hata hivyo matarajio hayo mapya yapo juu kidogo kutoka yale ya awali yalikuwa yamebainisha na Dk Mpango wakati akisoma bajati ya wizara yake.


Soma zaidi:


Awali Serikali ilikuwa imetarajia uchumi mwaka 2020 ungekua kwa wastani wa asilimia 4 kutoka kwenye matarajio ya asilimia 6.9 kutokana na madhara ya ugonjwa wa virusi vya corona kwenye shughuli za biashara na uchumi.

Ikumbukwe kuwa uchumi mwaka 2019 ulikuwa kwa wastani wa asilimia 7.

Enable Notifications OK No thanks