Ubunge jimbo la Arusha: Makonda, Gambo watupiana maneno 

February 25, 2025 5:29 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Gambo asema waliomtaka Makonda achukue fomu wametengenezwa.

Arusha. Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo amesema Madiwani wa Baraza la Halmashauri Arusha waliomtaka Mkuu mkoa huo Paul Makonda kugombea ubunge wa jimbo hilo wametengenezwa.

Februari 24 mwaka huu madiwani wa halmashauri hiyo walikutana kwa ajili ya kikao maalum cha kujadili bajeti ambapo pamoja na mambo mengine walimkata Makonda kuchukua fomu ya ubunge ili agombee katika uchaguzi wa Serikali Kuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Akizungumza na wanahabari leo Februari 25, 2024 Gambo amesema kuwa madiwani hao ambao hawazidi wawili wamepangwa ili kumuondoa madarakani baada ya kuzuia ubadhirifu wa Sh252 milioni uliotaka kutokea katika ununuzi wa eneo la Serikali litakalotumika kujenga shule.

“Nilipata taarifa kwamba ndugu Paul Makonda alihudhiuria kikao hicho (cha madiwani) na dalili zote zinaonesha kwamba kuna watu wake aliokuwa amewatengeneza ili waweze kuzungumza hayo masuala ambayo yamezungumzwa,” amesema Gambo.

Kwa mujibu wa Gambo jiji hilo lilitaka nunua eneo la heka sita  kwa ajili ya ujenzi wa shule kwa gharama ya Sh300 milioni lakini baadhi ya watu walichelewesha ununuzi wa eneo hilo kwa maslahi binafsi wakitaka kuliuza kwa Sh552 milioni.

Baada ya kupata msaada kutoka taasisi nyingine eneo hilo lilinuliwa kwa gharama halisi huku kukiwa na nyongeza ya ekari moja jambo lililowakera baadhi ya watu hao kiasi cha kutamani kumtoa madarakani kwa kumshinikiza Makonda achukue fomu.

“Katika hali ya kawaida ni lazima wajisike vibaya lazima wachanganyikiwe na hawana namna yoyote ya kunifanya chochote wakaona fursa pekee waliyokuwa nayo ni kumuita ndugu Paul Makonda waweze kutoa kiu yao na wanajulikana hawazidi watu watatu wanne,” amesema Gambo.

Kwa upande wake Makonda aliyekuwa akizungumza kwenye mkutano huo wa bajeti wa madiwani wa halmashauri kuu amesema anafahamu kuhusu sakata hilo la ubadhirifu wa Sh252 milioni na kuagiza waliohusika wachukuliwe hatua.

“Nataka mkoa wa Arusha kuwa namba moja kwa kila kitu. Hatuwezi kukubali kupunguza mapato, tunataka kuongeza mapato ili maendeleo yaweze kufanyika katika kila kata…

…Nimeiona hiyo taarifa ya upotevu wa fedha hizo jana zinazodaiwa kupi gwa nataka nipate majibu ,yaani nikupanga fitina tu na majungu na kama jambo huna uhakika nalo tuambie tuchukue hatua tusitukie majukwaa ya kisiasa kuleta fitina,” amesema Makonda.

Pamoja na hayo Makonda alimtaka Gambo kuhudhuria vikao vya halmashauri na kuacha kutoa taarifa za ndani ya halmashauri hiyo katika mikutano ya hadhara.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV