TRC: Hitilafu ya kiuendeshaji chanzo ajali ya SGR
- Yasema uchunguzi wa kina na juhudi za kuhakikisha kwamba huduma zinarejea haraka zinaendelea
Dar es Salaam. Shirika la Reli nchini (TRC) limesema hitilafu ya kiuendeshaji ndoo chanzo cha ajali ya treni ya umeme iliyokua ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma majira ya saa 2:00 asubuhi leo Oktoba 23, 2025 .
Ajali hiyo imetokea kituo cha Ruvu na kwa taarifa za awali hakuna tukio la kifo.
Taarifa ya TRC iliyotolewa na Mkurugeni Mkuu Mhandisi Machibya Shiwa, imeeleza kuwa kwa sasa timu ya wataalamu ikiongozwa na Katibu Mkuu Uchukuzi, vyombo vya ulinzi na usalama na menejimenti ya TRC inaendelea na uchunguzi wa kina na juhudi za kuhakikisha kwamba huduma zetu zinarejea haraka
Aidha, TRC imeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwa abiria kutokana na ajali hiyo.
Hii ni ajali ya kwanza iliyohusisha mabehewa matatu kuhama nje ya reli, awali zilikuwa zikiripotiwa hitilafu zinazodaiwa kuwa za umeme ambapo safari zilikuwa zikisimama kupisha matengenezo na kisha safari kuendelea.
Latest



